Jumamosi, 06 Januari, 2024
Leo ni Jumamosi tarehe 23 Jamadithani 1445 Hijria sawa na 6 Januari 2024 Miladia.
Siku kama ya leo miaka 1238 kulingana na kalenda ya Hijria Tahir Dhulyaminayn mmoja wa makamanda wa utawala wa Bani Abbas aliuawa. Tahir bin Hussein Dhulyaminayn alikuwa mmoja wa makamanda watajika wa Harun na Maamun. Aliteuliwa na Maamun kwa ajili ya kukabiliana na Ali bin Issa, kamanda wa Amin Abbasi na kumshinda na kishha akaikomboa Baghdad. ***
Siku kama ya leo 163 iliyopita ilianzishwa nchi ya Romania. Mpango wa kuasisiwa nchi ya Romania ulibuniwa tarehe 13 Disemba 1859 kwa kuunganishwa miji miwili midogo ya Moldavia na Wallachia. Miaka miwili baadaye majimbo na miji mingine ilijiunga na umoja huo na kuundwa nchi ya Romania. ***
Katika siku kama ya leo miaka 105 iliyopita, Theodore Roosevelt, Rais wa zamani wa Marekani aliaga dunia. Alizaliwa Oktoba 27 mwaka 1857 na alikuwa Rais wa 26 wa Marekanii. Alianza kuujihusisha na harakati za kisiasa tangu akiwa katika rika la ujana na baada ya kuwa mwanachama wa chama wa Repulican aliteuliwa kuwa makamu mwenyekiti wa chama hicho. ***
Katika siku kama ya leo miaka 64 iliyopita alifariki dunia Ali Isfandiyari mashuhuri kwa jina la Nima Yushij mwasisi wa mashairi ya kisasa nchini Iran. Isfandiyari alizaliwa katika mojawapo ya vijiji vya mkoa wa Mazandaran kwa jina la Yush huko kaskazini mwa Iran. Malenga huyo baadaye alielekea Tehran na kuanza kujifunza lugha ya Kifaransa. Nima Yushij alianza kutunga mashairi na kubuni mfumo mpya wa mashairi. Miongoni mwa sifa za mfumo huo wa mashairi mapya ni kueleza masuala ya jamii kwa lugha nyepesi na kutokuwa na wizani. Kazi muhimu zaidi ya malenga huyo mashuhuri wa Iran ni maarufu kwa jina la "Afsaneh". ***
Siku kama ya leo miaka 42 iliyopita kulitokea hamasa ya mashahidi wa Huweize iliyoongozwa na Shahidi Alamul Huda katika miezi ya mwanzoni mwa uvamizi wa Iraq dhidi ya ardhi ya Iran. Mwezi Dei mwaka 1359 Hijria Shamsia na baada ya jeshi la Iran ya Kiislamu kuvishinda vikosi zaidi ya viwili vya jeshi la Iraq huko kusini mwa eneo la Susangerd, kundi moja la Jeshi la Sepah la Ahwaz huko kusini mwa Iran lilitumwa katika mji wa Huweize kwenda kuulinda mji huo mbele ya mashambulizi ya Iraq. Hata hivyo kutokana na kuchelewa kufika zana na hujuma kubwa ya Iraq, jeshi la Iran lililazimika kurudi nyuma. Wakati huo zaidi ya wapiganaji mia moja wa Jeshi la Sepah, wapiganaji wa kujitolea na wanafunzi wa vyuo vikuu wafuasi waaminifu wa Imam Khomeini wakiongozwa na Sayyid Muhammad Hussein Alamul Huda walibakia katika mji huo wa Huweize wakipambana na adui na wakauawa shahidi. Baadaye jeshi la Iraq liliuvunja kabisa mji wa Huweize na kuusawazisha na ardhi. Pamoja na hayo ushujaa wa vijana hao shupavu wa Iran waliosabilia roho zao kulinda ardhi ya Jamhuri ya Kiislamu umebakia hai katika historia ya Iran. **
