Feb 09, 2024 22:57 UTC
  • Jumamosi, 10 Februari, 2024

Leo ni Jumamosi 29 Rajab 1445 Hijria ambayo inasadifiana na 10 Februari 2024 Miladia.

Siku kama ya leo, miaka 1169 iliyopita, alifariki dunia Abdullah bin Muslim Dinavari, maarufu kwa jina la Ibn Qutaybah akiwa na umri wa miaka 63. Ibn Qutaybah alizaliwa Kufah nchini Iraq na kushika cheo cha ukadhi huko Dinavar, magharibi mwa Iran. Alitabahari katika Qur’ani, Hadithi, mashairi na fasihi. Alimu huyo ameandika vitabu mbalimbali katika elimu za Kiislamu maarufu zaidi vikiwa ni “Ta’awiilu Mushkili-Qur’ani”, “Tafsiru Ghariibul-Qur’an”, “Uyunul-Akhbaar”, “Maani ash-Shi’ir” na “Gharibul- Hadith.” ***

Abdullah bin Muslim Dinavari, maarufu kwa jina la Ibn Qutaybah

 

Katika siku kama ya leo miaka 566 iliyopita, Shamsuddin fakihi na mfasiri wa Kiislamu wa Halab moja ya miji ya Syria aliaga dunia. Shamsuddin  alijifunza fikihi na tafsiri ya Qur'an kwa Ibn Hammam, fakihi na mwanazuoni mahiri wa zama hizo na kufanikiwa kuandika vitabu vyenye thamani katika uwanja huo. ***

Siku kama ya leo miaka 261 iliyopita ulitiwa saini mkataba baina ya Uingereza na Ufaransa katika mji wa Paris. Wafaransa waliutaja mkataba huo kuwa mbaya sana. Hii ni kutokana na kuwa, baada ya miaka mingi ya vita na mivutano na Uingereza, Ufaransa ilikubali kufumbia macho madai yake yote na maslahi yake ya kikoloni huko India na Canada. Sababu ya kutiwa saini mkataba huo ni kwamba, katika kipidi hicho Ufaransa ilikuwa imedhoofika kutokana na kujihusisha na vita mbalimbali barani Ulaya, na kwa upande wa kijeshi na kiuchumi haikuwa na ubavu wa kuendelea kupigana vita na Uingereza. ***

 

Siku kama ya leo miaka 133 iliyopita alifariki dunia Sophia Krukovsky mwanahisabati wa Russia. Alizaliwa mwaka 1850 mjini Moscow. Licha ya kuwa alipendelea sana elimu ya hisabati, lakini kutokana na sababu za kibaguzi hakuweza kujiunga na chuo kikuu na ni kwa msingi huo ndio maana akaelekea nchini Ujerumani na kujifunza elimu ya hisabati na fizikia. amoja na hayo Sophia Krukovsky alikabiliwa na matatizo mengi kabla ya kufanikiwa kujiunga na chuo kikuu. Kufuatia hali hiyo alilazimika kusoma elimu hiyo kwa mwalimu wa hisabati nje ya chuo kikuu. Mwaka 1874 Sophia Krukovsky alitunukiwa shahada ya juu ya Uzamivu (PhD) bila kuhudhuria chuoni. Mwaka 1888 alitunukiwa zawadi yenye itibari katika chuo cha academia nchini Ufaransa. Kuanzia mwaka 1884 hadi mwaka 1891 alipofariki dunia alijishughulisha na kazi ya ufundishaji wa hisabati katika Chuo Kikuu cha Stockholm, Sweden. ***

Sophia Krukovsky

 

Katika siku kama ya leo miaka 77 iliyopita, tawala za waitifaki na zile zilizokuwa zikihasimiana katika Vita vya Pili vya Dunia zilisaini makubaliano ya amani. Katika siku hiyo, Marekani, Urusi ya zamani, Uingereza na Ufaransa zilisaini makubaliano ya amani na nchi zilizoshindwa katika vita hivyo yaani Italia, Finland, Poland, Hungary, Romania na Bulgaria, na kwa utaratibu huo nchi sita hizo kwa mara nyingine tena zikajipatia uhuru. ***

Makubaliano ya amani baina ya madola waitifaki na zilizoshindwa katika Vita vya Pili vya Dunia

 

Siku kama ya leo miaka 45 iliyopita majenerali wa utawala wa Shah waliongeza muda wa serikali ya kijeshi katika mji wa Tehran. Majenerali hao walichukua hatua hiyo ili kuwazuia wananchi kuwaunga mkono na kuwasadia wanajeshi wa kikosi cha anga ambao walikuwa wakishambuliwa na kikosi cha gadi ya Shah, na kwa njia hiyo waweze kumtia mbaroni Imam Khomeini Mwenyezi Mungu amrehemu pamoja na shakhsiya wengine muhimu waliokuwa katika harakati za Mapinduzi au kuwauwa. Hata hivyo Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa kuona mbali na kusoma vyema alama za nyakati, aliwatolea mwito wananchi kupuuza kizuizi hicho kilichowekwa na majenerali wa Shah cha kuongeza muda wa serikali ya kijeshi au sheria za kutotoka nje. Wananchi wanamapinduzi wa Iran pia waliitikia agizo hilo la Imam Khomeini Mwenyezi Mungu amrehemu na kumininika katika mitaa mbalimbali na kueneza mapambano yao katika vituo vingine vya kijeshi vya utawala wa kidikteta wa Shah katika mji wa Tehran na miji mingineo.  ***

Shirika la Intelijensia na Usalama la utawala Shah lililokuwa maarufu kkwa jina la SAVAK,