Jumamosi, 16 Machi, 2024
Leo ni Jumamosi 5 ya mwezi mtukufu wa Ramadhani 1445 Hijria sawa na 16 Machi 2024 Miiladia.
Katika siku kama ya leo miaka 209 iliyyopita kwa mujibu wa kalenda ya Hijria, alizaliwa HHaj Mulla Ali Aliyari Tbarizi, mmoja wa maulamaa na wanazuoni mahiri wa Kiirani. Msomi hhuyu alizaliwa katika mji wa Tabriz moja ya miji ya kaskazini magharibi mwa Iran. Aliyari alibonea mno katika ellimu za fikihi na Usuul-Fiqh. Anahesabiwa kuwa mmoja wa wanafunzi wa Sheikh Murtadha Ansari na Mirza Shirazi. ***
Siku kama ya leo miaka 84 iliyopita, alifariki dunia Bi Selma Lagerlof mwandishi wa Sweden. Lagerlof alizaliwa mwaka 1858 na baada ya kumaliza masomo yake akaanza kujishughulisha na ukufunzi na uandishi wa hadithi na hekaya. Lagerlof alikuwa mwanamke wa kwanza kutunukiwa tuzo ya Nobel katika taaluma ya fasihi mwaka 1909. ***
Siku kama ya leo miaka 47 iliyopita, Kamal Fouad Jumblatt mwanasiasa mahiri wa Lebanon aliuawa. Alizaliwa Disemba 6 mwaka 1917 huko Moukhtara kusini mwa Beirut. Mwaka 1952 na kuendelea, Kamal Fouad Jumblatt alikuwa mwanasiasa wa mrengo wa upinzani na akafanikiwa kumuondoa madarakani Bechara El Khoury Rais wa muda wa wakati huo wa Lebanon. Hatimaye Kamal Fouad Jumblatt aliuawa na wapinzani wake katika siku ma ya leo akiwa na umri wa miaka 60. ***
Katika siku kama ya leo miaka 28 iliyopita, sawa na tarehe 26 mwezi Esfand mwaka 1373 Hijria Shamsia aliaga dunia Hujjatul Islam Walmuslimin Sayyid Ahmad Khomeini, mwana wa Imam Ruhullah Khomeini, (RA), mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Sayyid Ahmad Khomeini alizaliwa mwaka 1324 Hijria Shamsiya katika mji mtukufu wa Qum nchini Iran na kuanza kujifunza elimu ya kidini kwa baba yake. Sayyid Ahmad Khomeini alikuwa na nafasi muhimu katika kuwaunganisha wanamapinduzi na Imam Khomeini wakati wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. ***