Jumamosi, 21 Disemba, 2024
Leo ni Jumamosi 19 Mfunguo Tisa Jamadithani 1446 Hijria sawa na 21 Disemba 2024 Miladia
Siku kama ya leo miaka 649 iliyopita, "Giovanni Boccaccio" mwanafasihi na mwandishi maarufu wa Italia aliaga dunia. Giovanni Boccaccio, alizaliwa mnamo Septemba 8, 1313, karibu na Florence, Italia. Alikuwa na mchango mkubwa katika fani ya fasihi na alifanikiwa kutoa athari yake yak kwanza akiiwa katika rika la ujana.

Katika siku kama ya leo miaka 200 iliyopita alifariki dunia tabibu na mtaalamu wa masuala ya ardhi wa Uingereza, James Parkinson. Alijifunza tiba kwa baba yake na alikuwa wa kwanza kueleza kwamba ugonjwa wa appendix unaweza kusababisha kifo. Parkinson aligundua ugonjwa wa Parkinson na namna unavyotokea. Kwa sababu hiyo ugonjwa huo ulipewa jina la tabibu huyo. Dalili za ugonjwa huo ni kama vile kutetemeka sana na kwa muda mrefu kwa ulimi, kichwa na mikono na kushindwa kuvuta miguu wakati wa kutembea hususan katika kipindi cha uzeeni na pia kukakamaa misuli katika sehemu yoyote ya mwili. Ugonjwa wa Parkinson unasababishwa na baadhi ya matatizo katika ubongo na hadi kufikia sasa hakuna dawa mujarabu iliyopatikana kwa ajili ya kutibu maradhi hayo.

Miaka 85 iliyopita katika siku kama ya leo, aliaga duniia Allama Sayyid Nasser Hussein Musawi Hindi, fakihi na mtaalamu wa elimu ya hadithi. Sayyid Nasser Husseiin Hindi mwenye lakabu ya Shamsul-Ulamaa ni mtoto wa Sayyid Hamid Hussein mmoja wa wanazuoni wakubwa wa India na Mufti na Marjaa wa Iindia. Mbali na kubobea katiika fikihi na elimu nyinginezo alikuwa mahirii pia kkatika fani ya utunzi wa mashairi.

Siku kama ya leo miaka 36 iliyopita, watu 270 walipoteza maisha yao baada ya ndege ya abiria ya Marekani kuripuka katika anga ya Lockerbie huko Scotland. Marekani na Uingereza ziliwatuhumu raia wawili wa Libya kuwa ndio waliotega bomu katika ndege hiyo. Kufuatia mashinikizo ya nchi mbili hizo, mwaka 1992, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliiwekea vikwazo vya mafuta, anga na kijeshi nchi ya Libya, kwa tuhuma za kuwaficha Walibya hao. Hata hivyo kufuatia makubaliano kati ya Washington na serikali ya Tripoli, mwaka 1999 watuhumiwa hao walikabidhiwa kwa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai yenye makao yake makuu mjini The Hague, Uholanzi ambapo baada ya kesi hiyo mmoja kati ya watuhumiwa hao aliachiliwa huru baada ya kutopatikana na hatia, na wa pili alihukumiwa kifungo cha maisha jela.

Miaka 11 iliyopita katika siku kama ya leo, Ahmed Asmat Abdel-Meguid, Katibu Mkuu wa zamani wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 90. Ahmed Asmat Abdel-Meguid aliyekuwa mwanadiplomasia wa Kimsri alizaliwa mwaka 1923 katika mji wa Alexandria nchini Misri. Aliongoza Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kuanzia mwaka 1991-2001. Kabla ya kuchaguliwa kushika wadhifa huo, Ahmed Asmat Abdel-Meguid alikuwa Waziri wa Mashauuri ya Kigeni wa Misri kuanzia 1984 hadi 1991. Aidha mwaka 1985 alishika wadhifa wa Naibu Waziri Mkuu. Kadhalika Ahmed Asmat Abdel-Meguid aliwahi kuwa balozi wa Misri nchini Ufaransa na mwakilishi wa nchi hiyo katika Umoja wa Mataifa.
