Mazungumzo na Iran yameonyesha wazi kuwa Marekani ililenga kuhadaa
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i137140-mazungumzo_na_iran_yameonyesha_wazi_kuwa_marekani_ililenga_kuhadaa
Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje ya Iran na ambaye sasa ni mbunge amesema kuwa mazungumzo yameonyesha kuwa Marekani imekuwa ikifuatilia sera ya hadaa.
(last modified 2026-03-04T03:59:43+00:00 )
Mar 04, 2026 03:59 UTC
  • Manoucher Mottaki
    Manoucher Mottaki

Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje ya Iran na ambaye sasa ni mbunge amesema kuwa mazungumzo yameonyesha kuwa Marekani imekuwa ikifuatilia sera ya hadaa.

Manoucher Mottaki ameyasema hayo katika mazungumo na Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB) ambapo ameashiria mazungumzo ambayo yamekuwa yakifanyika kwa njia isiyo ya moja kwa moja kati ya Iran na Marekani chini ya upatanishi wa Oman.

Ameongeza kuwa: Wengi walijaribu kumzuia rais Trump wa Marekani kuanzisha vita, lakini waziri mkuu wa utawala wa Israel Netanyahu alikutana naye mara saba ili kumshawishi aanzishe vita.”

Amesema Trump alidhani kwamba ikiwa Kiongozi Muadhamu na makamanda wa ngazi za juu jeshini watauawa, hali itavurugika na Jamhuri ya Kiislamu itashindwa lakini njama hiyo imesambaratika.

Kwingineko katika mahojiano hayo, Mottaki amesema: “Siku hizi, jina la Imam Khamenei ambaye ni Imamu wa Mashahidi linatambulika kwa adhama na ukamilifu nchini Iran na duniani kote.” Amesema shahidi Imam Khamenei, aliyeuawa Jumamosi katika hujuma ya kigaidi ya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel alikuwa na uelewa wa juu katika sera za kigeni.