Sep 19, 2016 04:56 UTC
  • Wimbi la utakfiri katika ulimwengu wa Kiislamu sehemu ya (36)

Ni matumaini yangu kuwa hamjambo wapenzi wasikilizaji na karibuni tena katika mfululizo wa vipindi hivi vinavyoangazia macho chimbuko la makundi yenye kuwakufurisha Waislamu wengine na kutekeleza jinai na mauaji ya kutisha dhidi yao hii leo ikiwa ni sehemu ya 36 ya vipindi hivyo.

Hata hivyo pamoja na matukio yote hayo, nchi hizo za Kiarabu zikiongozwa na Saudia bado hazijapata funzo wala ibra. Hii ni kusema kuwa, nchi hizo bado zimeendelea kusimama dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zikisubiri kutoa pigo kwa nchi hii wakati wowote zitakapoweza. Katika mwenendo huo, Marekani na maadui wengine wa Iran ya Kiislamu wakaendeleza propaganda za kuchafua sura ya Iran kimataifa sanjari na kuielezea nchi hii kuwa ya hatari katika eneo la Mashariki ya Kati. Chuki hiyo dhidi ya Iran ilitekelezwa katika hatua kadhaa, ikiwemo za kijeshi kisiasa na kiutamaduni. Ni hapo ndipo maghala ya kuhifadhia silaha ya nchi za Kiarabu hususan Saudia yakajaa silaha na zana na kijeshi kutoka Marekani na Ulaya. Katika upande wa kisiasa, Saudia na baadhi ya waitifaki wake katika eneo la Mashariki ya Kati na kimataifa ikawa mtekelezaji siasa hizo za Marekani na Magharibi kwa ajili ya kuitenga kisiasa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran siasa ambazo zinaendelea hadi leo.    Katika mwenendo huo, Marekani na maadui wengine wa Iran ya Kiislamu wakaendeleza propaganda za kuchafua sura ya Iran kimataifa sanjari na kuielezea nchi hii kuwa ya hatari katika eneo la Mashariki ya Kati. Chuki hiyo dhidi ya Iran ilitekelezwa katika hatua kadhaa, ikiwemo za kijeshi kisiasa na kiutamaduni. Ni hapo ndipo maghala ya kuhifadhia silaha ya nchi za Kiarabu hususan Saudia yakajaa silaha na zana na kijeshi kutoka Marekani na Ulaya. Katika upande wa kisiasa, Saudia na baadhi ya waitifaki wake katika eneo la Mashariki ya Kati na kimataifa zikawa mtekelezaji siasa za Marekani na Magharibi kwa ajili ya kuitenga kisiasa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Ama katika upande wa kiutamaduni pia mataifa hayo yanajaribu kuchafua sura ya Uislamu halisi wa Bwana Mtume (saw) unaofuatwa nchini Iran kupitia mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, huku zikijaribu kuutaja Uislamu wa Kiwahabi kuwa eti ndio Uislamu unaoendana na Qur'an na suna za Mtume. Katika ulingo huo, Aal-Saud wakawekeza kiasi kikubwa cha fedha ikiwemo kuanzisha shule na vituo vya mafunzo ya Kiwahabi katika ncho tofauti za Waislamu. Shule ambazo baadaye zilikuja kuzalisha wanachama wa makundi ya al-Qaidah na Taleban, ambao walikuwa wamejazwa fikra za taasubi na ugaidi. Ni kwa kuzingatia ukweli huo, ndio maana Saudia ikatajwa na walimwengu kuwa mwanzilishi mkuu wa makundi yanayowakufurisha Waislamu wengine na ya kigaidi duniani.  

 

Mwaka 1995 wanachama wa kundi la kitakfiri la Taleban na kwa msaada kamili wa shirika la upelelezi la Pakistan, walifanikiwa kudhibiti sehemu kubwa ya ardhi ya Afghanistan ambayo wakati huo ilikuwa ikitawaliwa na serikali iliyokuwa ikiitwa Mujahidina. Wanachama wa Taleban wakaweka utawala wa karne za kati katika vijiji na miji waliyoitawala watu hao. Katika fremu hiyo wakapiga marufuku wasichana kwenda shule huku wanaume nao wakapigwa marufuku kushevu ama kupunguza ndevu zao. Kwa kosa dogo sana watu walikatwa miguu ama mikono yao. Kadhalika wanawake hawakuruhusiwa kutoka nje ya nyumba zao bila ya kujifunika gubigubi. Mbali na hayo matakfiri hao wa Kiwahabi wakatangaza uharamu wa matumizi ya vyombo vya teknolojia mfano wa televisheni, redio na mfano wa hayo. Kila siku wakawa wanatoa fatwa mpya na kuyafanya maisha ya raia wa nchi masikini ya Afghanistan kuwa magumu mno. Licha ya wanachama wa genge hilo kuweka utawala wa karne za kati katika maeneo mengi ya Afghanistan, hapakuwepo hata nchi moja ya Kimagharibi iliyokuwa tayari kulaani hatua za ukandamizaji dhidi ya ubinaadamu zilizokuwa zikifanywa na Taleban nchini humo. Kinyume chake baadhi ya viongozi wa Taleban walikuwa wakifanya safari katika miji mikuu ya nchi za Kiarabu na Magharibi bila tatizo lolote. Si nchi yoyote ya Magharibi hususan Marekani iliyotoa kauli ya kupinga hatua za wanachama wa Taleban waliokuwa wanaungwa mkono na Saudia na Pakistan nchini Afghanistan. Hii ni kwa kuwa wanachama hao walikuwa wakitekeleza ajenda za siasa za Marekani na Magharibi katika eneo la Mashariki ya Kati, kupitia waitifaki wa madola hayo, yaani Saudia na Pakistan. Hii ni katika hali ambayo, lau kama vitendo vya wanachama hao wa Taleban vikifanywa katika nchi ambazo sio waitifaki wa madola ya Magharibi, basi kungeibuliwa mawimbi ya propaganda katika ngazi mbalimbali za kisiasa na vyombo vya habari vya dunia. Ukweli ni kwamba, Taleban walikuwa wakiwasaidia Wamagharibi katika kuchafua sura ya Uislamu katika fikra za walio wengi duniani mkabala na Uislamu wa kupigania uadilifu, Amani, uhuru wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Leongo lao ilikuwa ni kuonyesha sura ya Uislamu wa kitakfiri wa kufanya ukatili na jinai dhidi ya binaadamu. Katika mazingira hayo Taleban na kwa uungaji mkono kamili wa Mawahabi wa Saudia wakafanikiwa kueneza Uislamu huo bandia kupitia vyombo vya habari vya nchi za Magharibi na Kiarabu, bila ya vyombo hivyo kulaani hata kidogo mienendo hiyo iliyo dhidi ya Uislamu halisi. Katika kipindi hicho, mtandao wa kundi la kigaidi la al-Qaaidah chini ya uongozi wa Osama Bin Laden ulikuwa ukiendeleza shughuli zake za siri nchini Afghanistan kupitia usimamizi kamili  wa mashirika ya  ujasusi ya nchi zile zile za Saudia na Pakistan. Kitendo cha Afghanistan kuangukia mikononi mwa wanachama wa al-Qaaidah, mara ikageuka na kuwa ngome ya kundi la al-Qaaidah. Kwa kipindi chote hicho al-Qaaidah walifanya jambo lolote walilolitaka ndani ya taifa hilo. Mwenendo huo uliendelea hadi mwaka 2001 baada ya kujiri shambulizi la kigaidi dhidi ya minara miwili ya kibiashara mjini New York na jingo la Wizara ya Ulinzi (Pentagon) nchini Marekani. Hadi wakati huo tayari makundi hayo ya Taleban na al-Qaaidah yalikuwa yamesaidia kufikiwa malengo ya Marekani na waitifaki wake katika eneo la Mashariki ya Kati hususan Saudia, kwa ajili ya kuhalalisha uingiliaji kijeshi wa Washington katika eneo kwa madai ya kile kinachosemwa kuwa ni kupambana na ugaidi. Kwa kipindi kilicho chini ya mwezi mmoja baada ya tukio hilo la Septemba 11 mwaka huo wa 2001, tarehe saba mwezi Oktoba rais wa wakati huo wa Marekani, George Walker Bush akatoa amri ya kushambuliwa kijeshi Afghanistan.  

Mmoja wa makamanda wakubwa wa ISIS (Daesh) aliyenyoa ndevu na kuvaa vazi la kike akiwa amekamatwa na maafisa usalama wa Iraq

 

Miaka miwili baadaye na kwa kisingizio cha kukabiliana na tishio la silaha hewa za nyuklia za dikteta Saddam Hussein wa Iraq na kadhalika ugaidi wa makundi ya al-Qaaidah na taleban, Marekani ikaivamia nchi hiyo hapo mwezi Machi mwaka 2003 ambapo Washington ilitumia askari wa baharini na nchikavu kurahisisha uvamizi huo. Hatua za viongozi wa Marekani katika kuivamia kijeshi Iraq, ilimalizika kwa kuzaliwa genge hatari la utakfiri na ugaidi la Daesh ambalo hii leo linaongoza kwa kutenda jinai dhidi ya binaadamu ndani na nje ya nchi hiyo. Ni kundi ambalo awali lilitangazwa kuwa tawi la mtandao wa al-Qaaidah. Hata hivyo baada ya kupita muda na kufuatia viongozi wa kundi hilo la Daesh kutowafuata vinara wa al-Qaaidah, kulipelekea kuibuka pengo kubwa baina ya wanachama wa makundi hayo mawili. Kama ilivyokuwa nchini Afghanistan madola ya Magharibi na Kiarabu yakajikita tena kufuatilia maslahi yao ya kisiasa nchini Iraq. Saudia ambayo baada ya kuondoka madarakani Saddam Hussein ilijawa na wasi wasi mkubwa kufuatia kuundwa serikali yenye asilimia kubwa ya Waislamu wa dhehebu la Shia, ilianzisha siasa za kuibua migogoro ndani ya nchi hiyo ya Kiarabu ya Iraq. Uungaji mkono kwa makundi ya kitakfiri na kigaidi ilikuwa hatua zilizopewa kipaumbele na watawala wa Aal-Saudi huko Iraq. Katika mazingira hayo, ndipo kukapatikana uhusiano wa karibu sana baina ya wanachama wa Ba'ath na makundi ya kitakfiri na kigaidi ya Daesh. Haukupita muda mara watu wenye fikra za kufurutu ada kutoka baadhi ya nchi za Kiarabu wakapelekwa nchini Iraq kwa ajili ya kile kilichosemwa kuwa ni kupambana na askari wa Marekani, ingawa kivitendo raia wa kawaida ndio waligeuka na kuwa wahanga wakubwa wa mauaji ya kujiripua na jinai kubwa za matakfiri na magaidi hao. Katika kipindi hicho, soko, mitaa na miji hususan ya Waislamu wa Kishia yakawa yakilengwa na operesheni za utegaji mabovu na kujiripua kwa matakfiri hao wasio na ubinaadamu mioyoni mwao. Ukweli ni kwamba watu hao wenye ya kufurutu ada ambao walikuwa wakifanya ukatili huo, hawakuwa na uelewa sahihi wa mafundisho ya dini ya Kiislamu, kutokana na mazingira waliyokulia, ambapo sanjari na kufuata mrengo wa siasa za kufurutu ada na taasubi, wanatumia nara ya dini kufikia malengo yao yasiyo ya kisheria na kupenda kujitanua na mali. Ama nukta muhimu ya kufaa kuzingatiwa katika kufafanua makundi hayo ya kitakfiri hususan Daesh ni juu ya nafasi ya nchi za Magharibi ikiwemo Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya katika kuundwa na kuyaunga mkono makundi hayo na kasha kuendelea harakati zake katika eneo la Mashariki ya Kati. Ndugu wasikilizaji, kundi la kigaidi la Daesh ni miongoni mwa makundi ya Kisalafi na kigaidi ambalo kwa kutumia fikra potofu za kitakfiri, linadai kutaka kuweka kile linachokidai kuwa ni 'Ukhalifa wa Kiislamu' nchini Iraq na Syria. Kundi hilo liliundwa tarehe 15 Oktoba mwaka 2006 nchini Iraq, kupitia kikao cha makundi kadhaa ya wabeba silaha nchini humo. Katika kikao hicho wajumbe walimteua Abu Omar al-Baghdadi, kuwa kiongoni wa genge hilo la kigaidi.   Wapenzi wasikilizaji kipindi cha makala ya utakfiri sehemu ya 34 kinakomea hapa kwa leo, msikose kusikiliza sehemu ya 37 ya makala haya wiki ijayo.