Apr 08, 2017 14:35 UTC

Hamjambo wapenzi wasikilizaji na karibuni kutegea sikio sehemu ya 31 ya mwisho kabisa wa makala haya yanayokosoa kwa mujibu wa Qur'ani Tukufu na suna za Bwana Mtume (sawa) mienendo ya makundi ya ukufurishaji yanayotenda jinai na mauaji ya kutisha dhidi ya Waislamu wengine.

Katika kipindi hiki cha mwisho tutakuleteeni maoni ya wasomi na wanafikra wa Kiislamu, kuhusiana na wimbi la makundi hayo.

Ndugu wasikilizaji, katika vipindi vyote vilivyopita, yaani kuanzia sehemu ya kwanza hadi ya 30 ya makala hizi, tulikuwa tukibainisha mienendo hasi na uelewa ghalati wa makundi ya kigaidi na ukufurishaji kunako mafundisho sahihi ya dini ya Uislamu. Tulisema kuwa, makundi ya kigaidi ambayo chimbuko lake ni Usalafi wa Kiwahabi wa nchini Saudia, hayana mafungamano yoyote na dini ya Uislamu, kama ambavyo pia hata jinai zinazofanywa na makundi hayo hazitakiwi kuhusishwa na Uislamu. Aidha licha ya makundi hayo ya kigaidi kutumia propaganda nyingi katika kujinasibisha na dini ya Kiislamu, ukweli ni kwamba, makundi hayo ni adui wa Uislamu na katika harakati zao, yanatekeleza mpango maalumu wa madola ya Magharibi, hususan Marekani, Uingereza, Ufaransa na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.

Wazalishaji na waliaji wa makundi ya kigaidi na ukufurishaji ya Kiwahabi

Mnafaa kufahamu kwamba, baada ya kumalizika kwa ukoloni wa kuzikalia kwa mabavu nchi mbalimbali kulikofanywa na madola ya Magharibi yanayopenda kujitanua, madola hayo hayakuwa na jinsi nyingine ghairi ya kuanzisha machafuko katika nchi makoloni yao ya zamani kwa lengo la kuendelea kupora raslimali za mataifa hayo. Katika fremu hiyo, ndipo madola hayo yakaanzisha makundi ya kigaidi yenye kufurutu ada ambayo awali yalianza kujitangaza kuwa yenyewe ndio yaliyoongoka ambayo wafuasi asi wake ndio wanaostahiki kuishi tu kwenye uso wa dunia.

Barack Obama, rais wa zamani wa Marekani, mwanzishi na mleaji wa magenge hatari ya kigaidi 

Kundi la Usalafi wa Kiwahabi (au Answar Suna) pia lilianzishwa katika ajenda hiyo hiyo ya kudhamini maslahi ya madola hayo ambapo tangu mwanzo wa kuasisiwa kwake hadi leo, limekuwa likihusika na machafuko na mauaji makubwa dhidi ya Waislamu wa Suni na Shia kupitia fatwa za ukufurishaji dhidi yao. Kuhusiana na suala hilo, Fadhli Mtani al-Nursi, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha jijini Morogoro anasema: “SAUTI .....”

*****************************************

Kwa kawaida matendo ya jinai yanayofanywa na makundi ya ukufurishaji ni lazima yapingwe na kila mtu mpenda haki na amani duniani. Ni kutokana na hali hiyo ili kujiepusha na lawama na katika kuhalalisha jinai zao, makundi ya kigaidi ndipo yakawa yanajinasibisha na dini ya Kiislamu ili kwa njia hiyo kuweza kuwahadaa walimwengu husan vijana wa Kiislamu waweze kujiunga nayo.

Mafuta ya nchi za Kiarabu yanayokodolewa macho na Wamagharibi

Hata hivyo swali la kufaa kujiuliza ni hili kwamba, wakati makundi hayo yakijinasibisha na dini ya Kiislamu, dini hiyo ilikuwa na msimamo upi msimamo kuhusiana na kadhia nzima ya kuwakufurisha Waislamu wengine sambamba na kufanya mauaji na jinai dhidi ya watu wasio Waislamu ambao hawana hatia? Kuhusiana na suala hilo, Sheikh Alhaj Baqir Mbwana, mwalimu mkuu wa shule ya Abi Dharr ya mjini Bububu, Zanzibar anasema: “SAUTI..2”

Aidha sehemu nyingine ambayo mbali na utekelezaji wa jinai dhidi ya Waislamu na watu wengine wasio kuwa Waislamu kunakofanywa na makundi ya Kisalafi na Kiwahabi, ni kueneza propaganda kubwa zenye lengo la kuwaonyesha walimwengu kwamba, jinai wanazozifanya dhidi ya wahanga wao, ni halali. Katika fremu hiyo na kupitia mitandao na kanali za televisheni zilizoasisiwa na kusimamiwa na madola ya Magharibi, Masalafi wa Kiwahabi na baadhi ya Masuni wenye uelewa mdogo wa masuala ya dunia au kwa kufuata maslahi ya dunia, wanawakufurisha Waislamu hususan wa Shia na kuwataja kuwa makafiri ambao wametoka nje ya Uislamu.

Waandamanaji wanaopinga vita vya Marekani nchini Syria

Kupitia propaganda hizo, huibua shubuhati mbalimbali ambazo hazina msingi wowote na Waislamu hao wa Shia, ilimradi kwa njia hiyo waweze kutekeleza mradi huo kabambe wa madola ya Kimagharibi. Huku hayo yakiwa hivyo kwa upande wa Masalafi wa Kiwahabi na Kisuni, wapo pia Waislamu wanaojinasibisha na Ushia ambao ima kutokana na elimu ndogo au kwa kuzingatia maslahi ya dunia, yanaingia katika mtego huo, ambapo kazi yao ni kutusi tu matukufu ya Waislamu wa Suni kwa lengo la kupalilia moto wa chuki na fitina dhidi ya Waislamu wa Shia.

Kanali ya Fadak ya Uingereza ambayo inatusi matukufu ya Waislamu wa Kisuni ili kueneza chuki

Katika hilo upande huo unapalilia chuki dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambayo ndio yenye asimilia kubwa ya Waislamu wa Shia duniani na kuwaonyesha Waislamu wengine kwamba kuwaua Mashia ni suala halali. Fadhli Mtani al-Nursi, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha jijini Morogoro anasema tena: “SAUTI ...3”

**********************************

Ndugu wasikilizaji eneo lingine ambalo linafuatiliwa na madola ya Magharibi katika kuchochea moto wa fitina wa makundi ya kigaidi na ukufurishaji ni kuwasahaulisha Waislamu, kunako kadhia muhimu ya Palestina.

Moja ya kanali za Kiwahabi zinazoeneza chuki dhidi ya Waislamu wa Mashia

Kwani wakati Waislamu wanapojikita katika kupigana wao kwa wao, ndivyo ambavyo kadhia ya Palestina inavyosahaulika katika fikra za Waislamu hao na ndivyo ambavyo utawala haramu wa Kizayuni wa Israela unavyoendelea kupora zaidi ardhi za Wapalestina na kujimilikisha wao binafsi. Wakati Waislamu walipoisahau kadhia hiyo walikumbwa na hali gani: Fadhli Mtani al-Nursi, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha jijini Morogoro anasema tena: “SAUTI 4”

Katika kumalizia, Sheikh Alhaj Baqir Mbwana, mwalimu mkuu wa shule ya Abi Dharr ya mjini Bububu, Zanzibar anaelezea umuhimu wa umoja baina ya Waislamu ambapo kwa kuzingatia suala hilo, hii leo Jamii ya Waislamu na Wasio kuwa Waislamu huko Zanzibar, wanaishi pamoja kwa upendo baina yao: “SAUTI 5..”

Ndugu wasikilizaji sehemu ya 31 na ya mwisho kabisa ya makala haya inakomea hapa kwa leo. Mimi ni Sudi Jafar. Was-Salaamu Alaykum warahmatullahi wa barakaatu…………./

 

Tags