Aug 26, 2017 22:07 UTC
  • Jumapili, Agosti 27, 2017

Leo ni Jumapili tarehe 5 Dhul-Qaadah mwaka 1438 Hijiria, sawa na tarehe 27 Agosti 2017 Miladia.

Siku kama ya leo miaka 1691 iliyopita mji wa Costantino katika kipindi cha utawala wa Roma ambao ndio kwanza ulikuwa umeasisiwa, uliteuliwa kuwa mji mkuu wa kistratijia wa ufalme huo upande wa mashariki. Mji huo ulijengwa na kupewa jina la mfalme yaani Constantinople, huko katika viunga mwa mashariki mwa ufalme huo. Hata hivyo muda punde baadaye ukabadilishwa jina hilo na kuitwa Constantino. Mwaka 1453 Miladia mji huo ulidhibitiwa na mfalme Muhammad wa utawala wa Othmania na kuuita jina la Istanbul. Inafaa kuashiria hapa kuwa, hii leo mji wa Istanbul ni mji uliofuka idadi kubwa ya watu nchini Uturuki.

Ramani ya mji wa Costantino

Siku kama ya leo miaka 382 iliyopita, alifariki dunia Lope de Vega, mwandishi mkubwa wa Uhispania. Vega alizaliwa mwaka 1562 Miladia na akiwa kijana mdogo alionekana kuwa mwenye harakati nyingi na mwenye kipawa kikubwa cha akili huku akianza pia kusoma mashairi. Akiwa na umri wa miaka 14 alijiunga na shule ya msingi na sekondari ya kidini ambapo baada ya kuhitimu masomo yake katika chuo kikuu, alijiunga na jeshi la kujitolea. Taratibu akaanza kuonyesha kipawa chake katika michezo ya kuigiza na masuala mengine na hivyo kuwavutia watu wengi. Lope de Vega anajulikana kuwa mwanzilishi wa michezo ya kuigiza kitaifa nchini Uhispani.

Lope de Vega,

Siku kama ya leo miaka 247 iliyopita, alizaliwa Georg Wilhelm Friedrich Hegel mwanafalsafa mkubwa wa Ujerumani. Licha ya msomi huyo kufundisha katika vyuo mbalimbali na kuandika vitabu tofauti, lakini bado alikuwa masikini. Kufuatia uvamizi wa jeshi la Napoleon dhidi ya Ujerumani mwaka 1806, Hegel alivutiwa na shakhsia ya kamanda huyo Kifaransa. Alibainisha hatua za historia na kuamiani kuwa, muelekeo wa harakati ya kihistoria huainishwa na Mwenyezi Mungu na kwamba hata malengo ya historia ni hivyo. Katika kubainisha itikadi yake, Georg Wilhelm Friedrich Hegel  aliandika vitabu kadhaa katika uwanja huo. Hegel alifariki dunia mwaka 1831 Miladia.

Georg Wilhelm Friedrich Hegel

Tarehe tano Shahrivar miaka 39 iliyopita kwa mujibu wa kalenda ya Kiirani, mwanzo wa kalenda ya Iran ulirejeshwa tena katika mwaka wa Hijria Shamsia kutoka mwanzo wa tarehe ya Kifalme. Katika miaka ya kabla ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu utawala wa kidikteta wa Pahlavi ambao ulitambua mafundisho ya Uislamu kuwa ni kinyume na maslahi yake, ulikuwa ukifanya njama za kukabiliana na Uislamu kwa kutumia utajiri na turathi ya kihistoria ya Iran. Katika mkondo huo bunge la kimaonyesho la utawala wa Kipahlavi lilipasisha sheria iliyobadilisha mwanzo wa kalenda ya Iran kutoka mwaka wa Hijra ya Mtume (saw) na kuifanya kuwa tarehe ya kuvikwa taji la Mfalme Kurosh wa silsila ya Khahamaneshi. Hatua hiyo lilikabiliwa na hasira na malalamiko makubwa ya Imam Ruhullah Khomeini na wananchi Waislamu wa Iran. Kubadilishwa huko kwa mwaka wa Hijria na kufuata mwaka wa Kifalme nchini hakukudumu kwa zaidi ya kipindi cha miaka miwili na nusu na utawala wa Shah uliokuwa ukikabiliwa na harakati za Mapinduzi ya Kiislamu ulilazimika kutambua tena mwaka wa Hijra ya Mtume (saw) kutoka Makka kwenda Madina kuwa ndiyo mwanzo wa kalenda nchini Iran. 

Mabadiliko ya kalenda ya Hijiria

Siku kama ya leo miaka 1187 iliyopita, yaani sawa na tarehe 5 Shahrivar alizaliwa Muhammad bin Zakaria Razi, msomi mkubwa wa ulimwengu wa Kiislamu. Ibn Zakaria Razi alizaliwa mwaka 251 hijria katika mji wa Rei nchini Iran na alianza kujifunza kemia na fizikia akiwa bado kijana. Tabibu na mkemia Muhammad bin Zakaria Razi alijifunza pia elimu nyingine kama vile tiba, mantiki na falsafa. Baadaye Razi alifanikiwa kutengeneza asidi ya sulfuriki kwa kustafidi na mada asilia. Msomi huyo wa Kiislamu Muirani alikuwa shakhsia wa kwanza kuvumbua alkoholi. Muhammad bin Zakaria Razi ameandika vitabu 56 vya tiba, 33 vya sayansi ya asili, 17 vya falsafa, 14 vya teolojia, 22 vya kemia na makumi ya vitabu vingine katika nyanja mbalimbali. Msomi huyo wa Kiislamu alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 60 na alizikwa katika mji wa Rei ambao hii leo uko kusini mwa Tehran.

Picha ya Muhammad bin Zakaria Razi

Siku kama ya leo miaka 77 iliyopita, alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 65 huko mjini Najaf, Iraq, Allamah Muhammad Hussein Gharawi Isfahani, maarufu kwa jina la 'Kampani', mwanafalsafa, mtaalamu wa sheria za Kiislamu na msomi mkubwa wa elimu ya irfani (ya kumjua Mwenyezi Mungu). Alizaliwa mwaka 1296 Hijiria mjini Kadhimiya nchini Iraq. Msomi huyo mtajika alikuwa na ufahamu mkubwa katika falsafa, hekima, irfani, historia, jografia, mashairi na fasihi. Aidha Allamah Muhammad Hussein Gharawi Isfahani anafahamika kwa kuwa na uwezo mkubwa wa kufikiri. Ameacha vitabu mbalimbali katika nyuga za fiqhi, falsafa na kadhalika.

Allamah Muhammad Hussein Gharawi Isfahani

Na siku kama ya leo miaka 211 iliyopita, yaani sawa na tarehe 27 Agosti mwaka 1806, jengo la kihistoria mjini Zanzibar linalojulikana kwa jina la Beit al-Ajaib lililojengwa na Sultan Barghash bin Said huko Forodhani Unguja, liliteketezwa kwa mizinga ya manowari za Uingereza. Hatua hiyo ilifuatia ugomvi uliozuka baina ya wana wawili wa Kifalme. Watoto hao walijulikana kwa majina ya Said Barghash Khalid na Said Hamud bin Muhammad. Watoto hao wa Kifalme walikuwa wakigombana kukitawala kisiwa cha Zanzibar. Vita hivyo vilidumu kwa dakika 45 tu na kuwa vita vifupi zaidi duniani.

Jengo la kihistoria mjini Zanzibar linalojulikana kwa jina la Beit al-Ajaib