Dec 02, 2017 05:52 UTC
  • Alkhamisi tarehe 30 Novemba, 2017

Leo ni Alkhamisi tarehe 11 Mfunguo Sita Rabiul Awwal 139 Hijria sawa na 30 Novemba, 2017.

Siku kama ya leo miaka 29 iliyopita, aliaga dunia katika mji wa Cairo Misri, Ustadh Abdul-Basit Abdul-Samad, mmoja wa waalimu na maqarii wakubwa wa Qur'ani Tukufu. Abdul-Basit alianza kujifunza Qurani Tukufu tangu akiwa mdogo na alipofikia umri wa miaka 12 akafanikiwa kupata tunzo ya kuhifadhi na kusoma Qur'ani. Ustadh Abdul-Basit katika maisha yake alijishughulisha na usomaji wa Qurani Tukufu na kutunukiwa zawadi na tunzo muhimu katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani tukufu kwenye nchi mbalimbali za Kiislamu, sambamba na kuwavutia Waislamu wengi kwenye kusoma maneno hayo ya Mwenyezi Mungu. Abdul Basit ameacha kanda nyingi za sauti yake nzuri ya Qur'ani Tukufu.

Abdul Bast Abdul Samad

Katika siku kama ya leo miaka 350 iliyopita, Jonathan Swift mwandishi mashuhuri wa Ireland alizaliwa huko Dublin mji mkuu wa nchi hiyo. Swift alishiriki pakubwa katika harakati za ukombozi wa Ireland. Baadae, Jonathan Swift alianza kujishughulisha na kazi ya uandishi. Swift alifariki dunia akiwa na miaka 78.

Jonathan Swift

Siku kama ya leo miaka 146 iliyopita alizaliwa mwanazuoni mkubwa wa Kiislamu Allamah Agha Bozorge Tehrani. Alipata elimu ya msingi mjini Tehran na baadaye alielekea Najaf, Iraq kwa ajili ya elimu ya juu. Allamah Agha Bozorge Tehrani alikweya kwa kasi daraja za elimu na kuwa miongoni mwa wanazuoni wakubwa wa kidini. Allamah Tehrani alisafiri na kufanya uchunguzi katika maktaba nyingi za nchi kama Iran, Misri, Syria, Iraq, Hijaz, Palestina na kadhalika kwa ajili ya kutayarisha ensaiklopedia ya vitabu vya Kiislamu. Alifanikiwa kuandika tabu hilo kubwa lenye juzuu 26 ambalo alilipa jina la "Adhari'a ila Tasaanifish Shia". Kitabu kingine muhimu cha Allamah Agha Bozorge Tehrani ni "Tabaqatu Aalami Shia" chenye juzuu 8. Msomi huyo mkubwa wa Kiislamu alifariki dunia katika mji mtakatifu wa Najaf na kuzikwa katika maktaba yake kama alivyokuwa ameusia.

Ayatullah Agha Bozorg Tehrani (katikai)

Siku kama ya leo miaka 200 iliyopita, alizaliwa Theodor Mommsen mwanahistoria na mtafiti wa Ujerumani. Baada ya kumaliza masomo, Mommsen alijishughulisha na utafiti kuhusiana na vitabu tofauti na athari zilizobakia za tamaduni za zamani. Miongoni mwa vitabu vyake maarufu zaidi ni kitababu kinachoitwa 'Historia ya Roma ya Kale' ambacho ni kitabu kamili cha historia kuhusiana na mji wa Roma. Mwanahistoria huyo wa Ujerumani alitunukiwa tuzo ya Nobel katika fasihi hapo mwaka 1902 Miladia na kufariki dunia mwaka mmoja baadaye, akiwa na umri wa miaka 86.

Theodor Mommsem