Nov 03, 2020 20:43 UTC
  • Jumatano tarehe 4 Novemba 2020

Leo ni Jumatano tarehe 18 Mfunguo Sita Rabiul Awwal 1442 Hijria sawa na Novemba 4 mwaka 2020.

Siku kama ya leo miaka 1441 iliyopita kulingana na kalenda ya Hijria, ilianza kazi ya ujenzi wa Msikiti wa Mtume mjini Madina ambao ni msikiti wa pili kwa utukufu duniani baada ya Masjidul Haram. Mtume (SAW) alitoa amri ya kujengwa msikiti wa Madina baada tu ya kuhamia mjini humo na yeye mwenyewe alishiriki katika ujenzi wake. Kandokando ya msikiti huo kulijengwa vyumba vya Mtume na baadhi ya maswahaba zake. Mtume hakuutumia msikiti kwa ajili ya ibada tu, bali alitumia pia sehemu hiyo kwa ajili ya masuala kama kutoa hukumu baina ya watu, vikao vya mashauriano, mafunzo ya kivita na utatuzi wa masuala mbalimbali ya Waislamu.

Masjidun Nabii

Siku kama ya leo miaka 75 iliyopita, Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO, liliundwa kwa ushirikiano wa nchi 43. Lengo la kundwa taasisi hiyo lilikuwa ni kuweka mawasiliano ya kielimu na kiutamaduni kati ya mataifa mbalimbali pamoja na kusambaza vitabu na makala kwa lugha mbalimbali duniani ili kwa njia hiyo kuwepo mafungamano ya kiutamaduni kwa mataifa ya dunia. Miongoni mwa nukta muhimu za kuvutia katika hati ya UNESCO ni kuheshimiwa uadilifu, sheria, haki za binadamu na uhuru wa mwanadamu. Shirika hilo la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa, linaundwa na nguzo tatu kuu muhimu ambazo ni Katibu Mkuu, Kamati ya Utendaji na Baraza Kuu.

Siku kama ya leo miaka 42 iliyopita, wakati wa kuendelea harakati za mapambano ya wananchi wa Iran dhidi ya utawala dhalimu wa Shah, serikali ya Sharif Emami ililazimika kujiuzulu. Jafar Sharif Emami alikuwa kibaraka wa ukoloni wakati wa kupamba moto harakati za wananchi Waislamu na alikuwa akitoa ahadi za uongo kwa lengo la kupotosha mwelekeo wa Mapinduzi ya Kiislamu. Baada ya Sharif Imami, Jenerali Azhari aliunda serikali ya kijeshi. Hata hivyo Imam Khomeini aling'amua njama na hila za kiongozi huyo na kutangaza kwamba, mawaziri wakuu wanaobadilishwa ni vibaraka wa Shah na ubeberu na akawataka wananchi wasihadaike na hila za viongozi hao bali waendeleze harakati za mapambano za kutaka kuangusha utawala dhalimu wa Shah.

Sharif Emami

Siku kama ya leo miaka 33 iliyopita kulifunguliwa maonyesho ya kwanza ya kimataifa ya vitabu mjini Tehran. Maonyesho hayo yalishirikisha makampuni na taasisi 196 za uchapishaji vitabu za kigeni kutoka nchi 32 duniani yaliyokuwa na vitabu zaidi ya elfu 16. Vilevile taasisi 215 za uchapishaji za ndani ya Iran zilishiriki katika maonyesho hayo. Tangu mwaka huo Maonyesho ya Kimataifa ya Vitabu ya Tehran yamekuwa yakifanyika kila mwaka hapa nchini.

Siku kama ya leo miaka 25 iliyopita, Yitzhak Rabin, Waziri Mkuu wa zamani wa utawala haramu wa Israel aliuawa na Mzayuni mwenye misimamo ya kufurutu ada. Rabin alikuwa Waziri Mkuu wa Israel kuanzia mwaka 1974 hadi 1977 kupitia tiketi ya Chama cha Leba. Hata hivyo aliuzuliwa katika wadhifa huo kwa tuhuma za ubadhirifu na ufisadi. Mwaka 1992 kwa mara nyingine tena Rabin alifanikiwa kuwa Waziri Mkuu na kuendelea na mazungumzo yaliyofahamika kwa jina la Amani ya Mashariki ya Kati. Aidha kuuawa Yitzhak Rabin na Mzayuni huyo mwenye kufurutu ada, kulidhihirisha tofauti za ndani katika utawala bandia wa Kizayuni.

Yitzhak Rabin