-
Taharuki Kenya huku matokeo ya uchaguzi wa urais yakisubiriwa kwa hamu
Aug 11, 2017 03:15Hali ya taharuki imetanda nchini Kenya huku Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini humo (IEBC) ikitazamiwa kumtangaza mshindi wa uchaguzi wa urais wakati wowote tokeo sasa hii leo.
-
Upinzani Kenya waitaka IEBC imtangaze Raila Odinga mshindi wa uchaguzi wa urais
Aug 10, 2017 10:47Mrengo wa upinzani wa NASA nchini Kenya umeitaka Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC imtangaze mgombea wa muungano huo Raila Odinga kuwa, mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika nchini humo siku ya Jumanne.
-
Watu 5 wameuawa katika ghasia za baada ya uchaguzi mkuu Kenya
Aug 10, 2017 04:18Watu 5 wameripotiwa kuuawa katika ghasia na machafuko ya baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika juzi nchini Kenya baada ya kinara wa kambi ya upinzani, Raila Odinga kudai kuwa kumefanyika udanganyifu mkubwa.
-
Igad: Uchaguzi mkuu Kenya umefanyika kwa amani, uwazi na utaratibu sahihi
Aug 09, 2017 11:41Timu ya wasimamizi wa uchaguzi ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiserikali wa Nchi za Mashariki na Pembe ya Afrika (Igad) imeipongeza Tume Huru ya Uchaguzi ya Kenya (IEBC) kwa kusimamia uchaguzi kwa njia sahihi na kusema kuwa, tume hiyo inapaswa kuwa kigezo cha kuigwa na nchi nyingine za Afrika.
-
Ngombea Urais akiri kushindwa Kenya, mmoja auawa kituo cha uchaguzi Kisii
Aug 09, 2017 10:29Mgombea urais wa kujitegemea katika uchaguzi mkuu wa Kenya amekiri kushindwa baada ya matokeo ya awali ya uchaguzi wa rais kuonesha kuwa, ameshika nafasi ya sita kwa kupata kura elfu 11 na 256.
-
Uhuru Kenyatta aongoza katika uchaguzi wa rais Kenya, upinzani wapinga matokeo
Aug 08, 2017 22:58Kinara wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amepinga matokeo ya awali ya uchaguzi wa urais uliofanyika jana Jumanne, yanayoonyesha kuwa Rais wa sasa Uhuru Kenyatta anaongoza.
-
Uchaguzi mkuu nchini Kenya
Aug 08, 2017 05:58Raia wa Kenya waliotimiza masharti ya kupiga kura Jumanne ya leo wameelekea katika vituo vya kupigia kura kwa ajili ya kumchagua Rais, madiwani, maseneta, wabunge, magavana na wawakilishi wa wanawake katika uchaguzi ambao unatajwa kuwa na ushindani mkubwa.
-
UN: Tunafuatilia kwa karibu uchaguzi wa Kenya
Aug 08, 2017 03:21Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema umoja huo unafuatilia kwa karibu zoezi la uchaguzi mkuu linalofanyika hii leo nchini Kenya.
-
Igad yataka kufanyika uchaguzi wa amani Kenya
Aug 08, 2017 00:09Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiserikali wa Nchi za Mashariki na Pembe ya Afrika (Igad) imewatolea wito washika dau wote katika uchaguzi mkuu wa Kenya kuhakikisha kuwa uchaguzi wa leo unafanyika kwa amani na utulivu.
-
Wakenya wakusanya akiba ya chakula kabla ya uchaguzi mkuu kesho Jumanne
Aug 07, 2017 12:11Wananchi wa Kenya ambao wamejawa na wasiwasi leo wamekuwa wakikusanya na kujiwekea akiba ya chakula huku polisi wakiwa tayari wameandaa masanduku ya huduma ya kwanza siku moja kabla ya uchaguzi mku wa kesho ambao wengi wanahofu kwamba huwenda ukaitumbukiza tena nchi hiyo katika hali ya mchafukoge.