Pars Today
Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn amesema nchi yake itaendelea kushirikiana na Somalia katika mapambano dhidi ya kundi la kigaidi na kitakfiri la al-Shabaab.
Watu wasiopungua saba, wengi wakiwa wanawake wakulima, wameuawa karibu na mji mkuu wa Somalia kufuatia hujuma ya kigaidi huku mji huo ukiwa bado unaomboleza shambulizi la hivi karibuni lililoua mamia ya watu.
Rais Mohammad Abdullahi Mohamed wa Somalia ameapa kupambana na kundi la kigaidi la al-Shabab kufatia hujuma mbaya zaidi ya kigaidi kuwahi kushuhudiwa katika mji mkuu wa nchi hiyo Mogadishu ambapo watu zaidi ya 300 waliuawa.
Aliyekuwa Naibu Kiongozi wa kundi la kigaidi na kitakfiri la al-Shabaab na pia msemaji wa zamani wa genge hilo Mukhtar Robow amelaani vikali shambulizii la kigaidi lililoua watu zaidi ya 300 katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu Jumamosi iliyopita.
Mripuko wa lori lililotegwa bomu ndani yake uliua watu wasiopungua 276 mjini Mogadishu, Somalia siku ya Jumamosi jioni.
Uturuki imefungua kituo chake kikubwa zaidi cha kijeshi barani Afrika ambacho kiko katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.
Magaidi wakufurishaji wa al-Shabab wameshambulia na kuteka kituo kimoja cha kijeshi karibu na mji mkuu wa Somalia, Mogadishu ambapo wanajeshi 15 Wasomali wameuawa katika tukio hilo.
Vijana wa Afrika wanajiunga na makundi yenye misimamo mikali kutokana na sababu kadhaa ikiwemo kupuuzwa, kunyimwa fursa pamoja na ukosefu wa utawala bora.
Kundi la kigaidi na kitakfiri la al-Shabaab limedai kuwa limeua makumi ya askari wa Somalia karibu na mji wa bandari wa Kismayu mapema leo Jumapili.
Watu 12 wameuawa katika shambulizi la bomu lililofanywa na genge la kigaidi na kitakfiri la al-Shabaab katika eneo lenye mamlaka ya ndani la Puntland nchini Somalia.