-
Hizbullah: Tutaamua 'wakati na mahala' pa kutolea jibu la mauaji ya Tabatabai yaliyofanywa na Israel
Nov 29, 2025 11:15Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya nchini Lebanon ya Hizbullah amesema, harakati hiyo ina haki ya kutoa jibu kwa shambulio la kigaidi lililofanywa na utawala wa kizayuni wa Israel lililomuua Kamanda wake mwandamizi Haytham Ali Tabatabai, na akaongeza kuwa Hizbullah yenyewe itaamua wakati na mahali pa kutolea jibu hilo.
-
Baada ya Israel kuwaua Wapalestina wengine 24 Ghaza, HAMAS yataka wapatanishi, hasa US iingilie kati
Nov 23, 2025 07:05Jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel limefanya mashambulizi makali ya anga katika maeneo tofauti ya Ukanda wa Ghaza, na kuwaua shahidi Wapalestina wasiopungua 24, wakiwemo watoto, katika mwendelezo wa ukiukaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyofikiwa tangu wiki sita zilizopita kwenye eneo hilo la Palestina lililoteketezwa kwa vita.
-
Nyaraka za jeshi la Israel zafichua: Mfungwa wa Kipalestina aliyebakwa alikuwa raia, si mpiganaji
Nov 04, 2025 11:18Waraka wa siri wa jeshi la Israel umefichua kwamba mtu aliyeshambuliwa kikatili na kubakwa na kundi la wanajeshi wa Israel katika gereza maarufu la Sde Teiman mnamo Julai mwaka jana hajawahi kushtakiwa kwa uhalifu wowote na alikuwa raia, kinyume na madai kwamba alikuwa na mwanachama harakati za mapambano ya Hamas.
-
Afisa wa Marekani aliyejiuzulu: Wanajeshi wa Marekani wanashiriki katika vita vya Israel huko Gaza
Jun 27, 2024 02:59Afisa aliyejiuzulu kutoka Shirika la Ujasusi la Ulinzi la Marekani, Meja Harrison Mann, amesema kuwa vita vilivyoanzishwa na Israel katika Ukanda wa Gaza havingeweza kuendelea hadi leo bila msaada usio na kikomo wa Marekani, akisisitiza kwamba wanajeshi wa Marekani wanapigana katika kuilinda Israel.
-
Mapambano yanaendelea kwa siku ya tatu, Hamas yapiga Ashkelon na Ashdod
Oct 09, 2023 15:03Mapigano kati ya wapigania ukombozi wa Palestina na jeshi la utawala vamizi wa Israel yameendelea leo kwa siku ya tatu katika maeneo ya ndani ya vitongoji vya walowezi wa Kizayuni karibu na Ukanda wa Gaza, ukiwa mwendelezo wa Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa iliyoanzishwa na Brigedi za Izzuddin Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu (Hamas) dhidi ya uvamizi wa Israeli, huku kukiwa na makadirio kwamba Wazayuni wasiopunguau 1,000 wa Israeli wameangamizwa hadi sasa.
-
UN: Mwanahabari Shireen Abu Akleh aliuawa na wanajeshi wa Israel
Jun 24, 2022 13:26Umoja wa Mataifa umesema taarifa ulizokusanya zinaonesha kuwa, Shireen Abu Akleh, mwandishi wa habari wa televisheni ya al-Jazeera ya Qatar aliuawa kwa kupigwa risasi na vikosi vya Israel.
-
Imarati yatakiwa kuangalia upya uhusiano, mapatano yake na Israel
May 08, 2021 12:20Muungano wa Muqawama Dhidi ya Kuanzishwa Uhusiano na Israel wa Umoja wa Falme za Kiarabu umeitaka serikali ya Imarati, wafanyabiashara na shakhsia huru wa nchi hiyo ya Kiarabu kuangalia upya mapatano ya ushirikiano yaliyofikiwa hivi karibuni baina ya UAE na utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Jumatatu Disemba 14 2020
Dec 14, 2020 03:00Leo ni Jumatatu tarehe 28 Mfunguo Saba Rabiuthani 1442 Hijria mwafaka na tarehe 14 Desemba 2020 Miladia.
-
Jeshi la Israel laua na kuwateka nyara vijana wa Palestina
Dec 04, 2018 14:37Wanajeshi katili wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamemfyatulia risasi na kumuua shahidi kijana wa Kipalestina aliyekuwa na umri wa miaka 22, katika hujuma ya leo asubuhi katika mji wa Tulkarem, Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
-
Jeshi la Israel laendeleza ukatili wake, laua Wapalestina 7 Gaza
Sep 29, 2018 08:13Kwa akali Wapalestina saba wameuawa shahidi huku wengine zaidi ya 500 wakijeruhiwa baada ya jeshi la Israel kuwamiminia risasi na kuvurumishia mabomu ya kutoa machozi waandamanaji wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza.