Dec 04, 2018 14:37 UTC
  • Jeshi la Israel laua na kuwateka nyara vijana wa Palestina

Wanajeshi katili wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamemfyatulia risasi na kumuua shahidi kijana wa Kipalestina aliyekuwa na umri wa miaka 22, katika hujuma ya leo asubuhi katika mji wa Tulkarem, Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Shirika la habari la Palestina la Wafa limeripoti kuwa, barobaro huyo wa Kipalestina kwa jina Mohammed Hossam Abdel Latif Habali ameuawa kwa kupigwa risasi kichwani na miguuni na kwamba alifariki dunia muda mfupi baada ya kufikishwa katika Hospitali ya Thabit mjini Tulkarem.

Kadhalika kijana mwingine wa Kipalestina anaendelea kupata matibabu katika eneo hilo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, baada ya kujeruhiwa kwa risasi za wanajeshi wa Kizayuni.

Wakati huohuo, vijana 10 wa Kipalestina wametekwa nyara na wanajeshi hao katili wa Israel katika operesheni iliyofanya usiku wa kuamkia leo katika miji wa Beitulah na Hebron, kusini mwa Ukingo wa Magharibi. Aidha wengine 9 wakiwemo watoto wawili wamekamatwa katika miji ya Nablus na Tubas, na watano katika miji ya Ramallah na Hizma, kaskazini mashariki mwa Quds.

Wanajeshi katili wa Israel wakikabiliana na waandamanaji wa Kipalestina Gaza

Mamia ya Wapalestina wameuliwa shahidi na askari wa Israel, maelfu ya wengine wamejeruhiwa huku wengine wengi wakikamatwa, tangu Baitul Muqaddas itangazwe kuwa mji mkuu wa utawala huo wa Kizayuni.

Licha ya upinzani mkubwa wa kieneo na kimataifa, manmo tarehe 6 Desemba mwaka uliopita wa 2017, Rais Donald Trump wa Marekani alitangaza kuwa Marekani inaitambua rasmi Quds (Jerusalem) kuwa mji mkuu wa Israel.

Tags