-
Ayatullah Hashemi Rafsanjani amezikwa leo
Jan 10, 2017 16:57Mwili wa marehemu Ayatullah Hashemi Rafsanjani, Mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu wa Iran umezikwa leo katika haram ya mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Imam Khomeini (MA).
-
Rais wa Russia atuma salamu za rambirambi kwa kifo cha Ayatullah Rafsanjani
Jan 10, 2017 16:42Rais Vladimir Putin wa Russia ametuma salamu za rambirambi na mkono wa pole kufuatia kifo cha Ayatullah Hashemi Rafsanjani, Mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Iran.
-
Viongozi mbali mbali duniani waomboleza kifo cha Ayatullah Rafsanjani
Jan 10, 2017 08:20Huku shughuli za kumzika Mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu hapa nchini, Ayatullah Akbar Hashemi Rafsanjani zikiendelea, shakhsia na viongozi mbali mbali wameendelea kutoa salamu zao za rambirambi kufuatia kifo cha mwanachuoni huyo.
-
Kiongozi Muadhamu aongoza Swala ya maiti ya Ayatullah Rafsanjani
Jan 10, 2017 08:20Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullahil Udhmaa Ali Khamenei ameongoza Swala ya maiti ya marehemu Ayatullah Akbar Hashemi Rafsanjani, rais wa zamani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Ayatullah Rafsanjani kuzikwa leo, Swala ya maiti inaongozwa na Ayatullah Ali Khamenei
Jan 10, 2017 04:35Ofisi ya Hamlashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu nchini Iran imetangaza kuwa, mwili wa marehemu Ayatullah Akbar Hashemi Rafsanjani utazikwa leo baada ya Swala ya maiti itakayoongozwa na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullahil Udhmaa Ali Khamenei.
-
Rais wa Algeria: Iran imepoteza kiongozi shujaa na mwana mwaminifu
Jan 10, 2017 03:46Rais Abdelaziz Bouteflika wa Algeria ametuma salamu za rambirambi kwa taifa la Iran kutokana na kifo cha aliyekuwa Mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu hapa nchini, Ayatullah Akbar Hashemi Rafsanjani.
-
Baadhi ya picha za Marhum Ayatullah Hashemi Rafsanjani katika matukio tofauti
Jan 09, 2017 17:00Hapa tumekuorodhesheeni baadhi ya picha alizopigwa Ayatullah Hashemi Rafsanjani, Mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwenye matukio tofauti. Ayatullah Rafsanjani amefariki dunia Jumapili tarehe 8 Januari 2017 akiwa na umri wa miaka 82
-
Rais wa Afrika Kusini atoa mkono wa rambirambi kufuatia kifo cha Ayatullah Rafsanjani
Jan 09, 2017 16:22Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ametoa ujumbe wa rambirambi kwa niaba ya Serikali na wananchi wa Afrika Kusini kufuatia kifo cha Ayatullah Hashemi Rafsanjani, Mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambaye pia ni Rais Mstaafu wa Iran na Spika Mstaafu wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran).
-
Shughuli ya kuuaga mwili wa Ayatullah Rafsanjani yafanyika na kuhudhuriwa na Rais Rouhani
Jan 09, 2017 08:02Shughuli ya kuuaga mwili wa Al-Marhum Ayatullah Hashemi Rafsanjani, Mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu imefanyika mapema leo kwa kuhudhuriwa na Rais Hassan Rouhani, viongozi mbalimbali wa vyombo vya serikali na vya ulinzi pamoja na wananchi wa matabaka tofauti.
-
Viongozi mbalimbali watoa salamu za rambirambi kwa Iran kufuatia kifo cha Ayatullah Rafsanjani
Jan 09, 2017 04:36Viongozi wa kisiasa wa nchi za eneo la Ghuba ya Uajemi wametoa salamu za rambirambi kwa taifa la Iran kufuatia kufariki dunia kwa Ayatullah Ali Akbar Hashemi Rafsanjani, Mkuu wa Halmashauri ya Kuanisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu Iran.