-
Wakimbizi wa Burundi waliopo Tanzania kuanza kurejea nyumbani Alhamisi hii
Oct 01, 2019 13:27Burundi leo imetangaza kuwa kundi la kwanza la wakimbizi wa nchi hiyo walioko Tanzania watarejea nyumbani Alhamisi wiki hii. Wakimbizi hao watarejea Burundi kwa umati kama sehemu ya mpango ulioratibiwa na serikali za nchi mbili hizo.
-
SAUTI, Mvutano kati ya Kanisa Katoliki na serikali ya Burundi washtadi, CNDD yahoji iwapo kanisa hilo nalo lina mgombea?
Sep 23, 2019 17:08Vutanikuvute kati ya serikali ya Burundi na Kanisa Katoliki imeendelea kushika kasi, huku mashirika yenye mafungamano na serikali yakilikosoa kanisa hilo na kuhoji iwapo linataka kusimika mgombea wake kwenye uchaguzi wa 2020.
-
AU yalaani mauaji ya askari wa Burundi nchini Somalia
Sep 18, 2019 02:39Umoja wa Afrika umelaani shambulizi la kigaidi dhidi ya askari wa kulinda amani wa Burundi waliokuwa wanahudumu chini ya mwavuli wa Kikosi cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (Amisom).
-
Umoja wa Mataifa watahadharisha kuhusu dhulma na ukandamizaji Burundi
Sep 05, 2019 07:45Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa wamesema katika ripoti yao waliyoitoa jana kuwa Burundi iko katika hatari ya kukumbwa na wimbi la ukandamizaji mpya wakati ikikaribia kuingia katika uchaguzi mkuu wa 2020. Taarifa hiyo imetolewa huku mgogoro wa kisiasa ulioigubika Burundi ukisalia bila ya ufumbuzi na nchi hiyo ikiwa na Rais anaendelea kujidhihirisha kuwa ni mtawala wa Kimungu.
-
Safari za meli baina ya Kigoma Tanzania na Bujumbura Burundi zaanza tena baada ya miaka 15 + Sauti
Aug 30, 2019 16:52Njia ya usafiri ya "Central Corridor" imezinduliwa rasmi kwa meli ya kwanza tangu miaka 15 kufika katika bandari ya Bujumbura Burundi kutokea Kigoma Tanzania, baada ya meli hiyo kusafirishwa kwa reli kutoka Dar es Salaam hadi Kigoma. Hamida Issa na maelezo zaidi kutoka Bujumbura.
-
Burundi na DRC zahimiza ushirikiano mkubwa zaidi baina yao + Sauti
Aug 28, 2019 07:01Meya wa jiji la Bujumbura na mkuu wa jimbo la kivu kusini mashariki mwa DRC wameafikiana kuimarisha ushirikiano ili kukabiliana na makundi ya watu wenye kubebelea silaha wanao hatarisha usalama mara kwa mara katika nchi hizi 2. Pia kuimarisha vita dhidi ya ugonjwa wa Ebola
-
Burundi yaanza kutoa chanjo ya Ebola kwa wahudumu wa afya
Aug 15, 2019 12:02Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa serikali ya Burundi imeanza kutoa chanjo ya virusi vya ugonjwa hatari wa Ebola kwa wahudumu wa afya hususan wale wanaofanyakazi karibu na mpaka wa nchi hiyo na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
-
SAUTI, Burundi yaadhimisha Siku ya Ziwa Tanganyika, kwa lengo la kulienzi ziwa hilo
Jul 26, 2019 15:11Nchi ya Burundi imeadhimisha Siku ya Kitaifa ya Ziwa Tanganyika kwa ajili ya kulienzi ziwa hilo.
-
Burundi yaadhimisha miaka 57 ya Uhuru + Sauti
Jul 01, 2019 16:06Leo Jumatano tarehe Mosi Julai 2019, Burundi imesherehekea mwaka wa 57 tangu ilipopata uhuru wake kutoka kwa mkoloni wa Ulaya, Ubelgiji. Rais Pierre Nkurunzinza ametumia fursa hiyo kutangaza hatua kadhaa ikiwa ni pamoja na kuondoa michango ya lazima kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2020. Hamida Issa na maelezo zaidi kutoka Bujumbura.
-
Jumatatu tarehe Mosi Julai 2019
Jul 01, 2019 01:32Leo ni Jumatatu tarehe 27 Shawwal 1440 Hijria sawa na tarehe Mosi Julai 2019.