-
Rais Rouhani: Waislamu wasimame kidete kutetea na kulinda thamani za Uislamu
Sep 11, 2020 04:46Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sambamba na kulaani kitendo cha jarida la Charlie Hebdo la Ufaransa cha kumvunjia heshima Mtume Muhammad SAW, ameyataka mataifa ya Kiislamu kusimama kidete kutetea na kulinda thamani, utamaduni na matukufu ya dini yao.
-
Kituo cha Kiislamu chachomwa moto Marekani siku ya kwanza ya Ramadhani
Apr 26, 2020 07:55Baraza la Uhusiano wa Kiislamu nchini Marekani (CAIR) limezitaka mamlaka husika nchini humo kuchunguza kitendo cha kuteketezwa kwa moto Kituo cha Kiislamu katika jimbo la Missouri, katika siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
-
Indhari ya Katibu Mkuu wa UN kuhusu uenezaji hofu na chuki dhidi ya Uislamu duniani
Feb 18, 2020 08:13Kujitokeza makundi ya kigaidi na yenye misimamo ya kufurutu mpaka na kuenea katika nchi za Magharibi vitendo vya kigaidi vinavyofanywa na makundi hayo, na vile vile kujitokeza mgogoro wa wakimbizi, ambao akthari yao ni Waislamu, yote hayo yametumiwa na baadhi ya viongozi na vyombo vya habari vya Magharibi kama kisingizio cha kueneza hofu na chuki dhidi ya Uislamu; jambo ambalo limeufanya Umoja wa Mataifa ulazimike kupaza sauti yake.
-
Guterres abainisha wasiwasi wake kuhusu kuongezeka chuki dhidi ya Uislamu duniani
Feb 17, 2020 07:48Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa anatiwa wasiwasi na kuongezeka vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu duniani na akasema mwenendo huo hauvumiliki.
-
Maelfu ya Waislamu waandamana Ufaransa kupinga chuki dhidi ya Uislamu
Nov 11, 2019 12:48Maelfu ya watu wameshiriki maandamano katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris kulalamikia chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu nchini humo.
-
Wiki ya Umoja wa Kiislamu-4: Nafasi ya Umoja katika kuepusha chuki dhidi ya Uislamu
Nov 11, 2019 10:33Katika ulimwengu wa leo chuki dhidi ya Uislamu, au kwa jila la kiingereza Islamophobia, ni jambo linalopewa uzito na kuenezwa kwa namna maalumu katika vyombo vya habari vya nchi za Magharibi.
-
Shambulizi dhidi ya msikiti Ufaransa; watu wawili wapigwa risasi
Oct 29, 2019 03:41Watu wawili wamejeruhiwa vibaya baada ya kupigwa risasi nje ya msikiti mmoja katika mji wa Bayonne, kusini magharibi mwa Ufaransa.
-
Mwanafunzi wa Kiislamu Marekani aondolewa mashindanoni kwa kuvaa hijabu
Oct 26, 2019 11:54Mwanafunzi wa kike wa shule moja katika jimbo la Ohio nchini Marekani ameondolewa kwenye mashindano ya mbio za nyika kwa kuvaa vazi la stara la hijabu.
-
Boris Johnson aushutumu Uislamu kuwa umezuia maendeleo katika baadhi ya maeneo duniani
Jul 16, 2019 12:03Mgombea anayeongoza katika kinyang'anyiro cha uwaziri mkuu wa Uingereza ametoa matamshi ya kuushutumu Uislamu kwa kudai kuwa dini hiyo ya Mwenyezi Mungu inazuia kupatikana ustawi na maendeleo katika jamii.
-
Waziri Mkuu wa Pakistan: Umma upambane na chuki dhidi ya Uislamu
Jun 01, 2019 11:25Waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan ametoa mwito kwa umma wa Kiislamu kupambana na dhulma na chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu duniani.