-
Indhari kali ya Ufaransa dhidi ya siasa za kibiashara za Trump
Jul 15, 2018 05:35Jean-Yves Le Drian, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa amekosoa siasa za kiuchumi zinazotekelezwa na Rais Donald Trump wa Marekani kuuhusu Umoja wa Ulaya.
-
Maandamano makubwa ya wananchi wa Uingereza wakipinga safari ya Trump mjini London
Jul 13, 2018 10:53Wimbi kubwa la wananchi wa Uingereza limefanya maandamano makubwa kupinga ziara ya Rais wa Marekani mjini London. Maandamano hayo yamefanyika kufuatia wito uliotolewa na taasisi za kutetea haki za binadamu na harakati zinazopinga vita za nchini humo.
-
Le Drian: Hatumruhusu Trump kuiyumbisha Ulaya
Jul 13, 2018 10:44Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa amekosoa siasa za kiuchumi zinazotekelezwa na Rais wa Marekani kuhusiana na Ulaya na kueleza kuwa, Paris haitatoa mwanya kwa Trump kuivuruga Ulaya.
-
Trump akaribishwa London kwa wimbi kubwa la maandamano
Jul 12, 2018 23:42Rais Donald Trump wa Marekani aliwasili London, mji mkuu wa Uingereza na kukaribishwa kwa wimbi kubwa la maandamano ya wananchi waliokuwa na hasira ambao wanapinga safari yake.
-
Trump aibua mifarakano katika muungano wa kijeshi wa NATO
Jul 12, 2018 05:03Siku ya kwanza ya kikao cha viongozi wa muungano wa kijeshi wa nchi za Magharibi, NATO, imemalizika huku mkutano huo ukishuhudia mashambulizi makali ya maneno ambayo hayajawahi kushuhudiwa ya Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya Ujerumani, moja kati ya nchi muhimu zaidi katika muungano huo wa NATO.
-
Kansela Merkel amjibu Trump na kumfahamisha kuwa Ujerumani huchukua maamuzi huru
Jul 11, 2018 09:11Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amejibu matamshi makali ya Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya nchi yake na kumfahamisha kuwa, 'Ujerumani inafuata sera na maamuzi huru'.
-
Marekani yalegeza msimamo wa vikwazo dhidi ya Iran baada ya kuonywa
Jul 11, 2018 08:51Marekani imelegeza msimamo wake mkali wa kuiwekea Iran vikwazo na kuzuia mafuta ghafi ya petroli ya nchi hii kuuzwa katika soko la kimataifa ifikapo Novemba 4.
-
Donald Tusk: Trump waheshimu washirika wa Marekani, huna marafiki wengi
Jul 10, 2018 23:46Mkuu wa Baraza la Umoja wa Ulaya, amemtaka Rais Donald Trump wa Marekani kuwa na heshima kwa washirika wa Washington na aache kuwakosoa kila siku.
-
Kuongezeka ukosolewaji wa siasa za Trump kuhusiana na suala la Korea Kaskazini
Jul 09, 2018 21:53Sambamba na kuanza tena vita vya maneno kati ya Marekani na Korea Kaskazini, ukosolewaji wa siasa za Rais Donald Trump kuhusiana na jinsi amekuwa akiamiliana na Korea Kaskizini umekuwa ukiongezeka.
-
Ukosoaji mkali wa Madeleine Albright dhidi ya siasa za Trump kuhusu JCPOA
Jul 09, 2018 08:01Akizungumza hivi karibuni na gazeti la Ujerumani la Der Spiegel Madeleine Albright, Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani wa Marekani amekosoa vikali hatua ya Rais Donald Trump wa nchi hiyo ya kujiondoka katika mapatano muhimu ya nyuklia ya JCPOA na kusema kuwa hatua hiyo inakinzana moja kwa moja na malengo aliyoyatangaza mwenyewe.