-
Msimamo mmoja wa kundi la 4+1 mbele ya madai hewa ya Marekani kuhusu Iran
Sep 21, 2020 07:03Licha ya Marekani kutoa madai hewa ya kuanza kutekelezwa vikwazo vya kimataifa dhidi ya Iran kuanzia jana Jumapili Septemba 20, 2020 vikiwemo vikwazo vya silaha, lakini mataifa ya dunia yamepinga madai hayo ya Washington na yamechukua msimamo imara kiasi kwamba inaonekana kama vile hakuna mabadiliko yoyote yaliyotokea.
-
Biden amtaka Trump ang'atuke madarakani
Sep 20, 2020 02:49Mgombea urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Democrat amemtaka rais wa nchi hiyo Donald Trump ang'atuke madarakani kwa sababu ya uongozi mbovu alioonyesha katika kukabiliana na virusi vya corona.
-
Afrika Kusini yakadhibisha tuhuma za Marekani dhidi ya Iran
Sep 19, 2020 06:34Baada ya Marekani kujiondoa katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, serikali ya Rais Donald Trump ilizidisha mashinikizo ya kiwango cha juu dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa shabaha ya eti kulemaza uchumi wa Iran na imekuwa ikitumia kila liwezekanalo kuanzisha vita vya kinafsi na kisaikolojia ikiwa ni pamoja na kutoa vitisho dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
-
Ilhan Omar: Trump ni dikteta na mbaguzi wa rangi
Sep 18, 2020 23:58Ilhan Omar, Mbunge mwanamke Muislamu katika Kongresi ya Marekani amesema, rais wa nchi hiyo Donald Trump ni mtu dikteta na mbaguzi wa rangi.
-
Shamkhani amwambia Trump: Wanaowaua Wairani watapelekwa jongomeo
Sep 17, 2020 03:41Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amejibu vitisho vilivyotolewa na Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya Iran na kusema: Wanaoamuru na watekelezaji wa mauaji ya wana wa Iran kama diteta wa zamani wa Iraq, Saddam Hussein na wengineo, watapelekwa jongomeo.
-
Zarif amwambia Donald Trump: Ni wakati wa kuamka
Sep 16, 2020 03:19Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amenusha propaganda chafu zinazofanywa na vyombo vya habari vya Magharibi kuhusu madai eti Iran inafanya mpango wa kumuua balozi Marekani nchini Afrika Kusini na kusema huu ni wakati wa kuamka.
-
Makanisa ya Wamarekani weusi: Trump anaunga mkono ugaidi wa wazungu
Sep 15, 2020 22:46Viongozi wa kanisa la Wamarekani wenye asili ya Afrika (AME) wamemtuhumu Rais wa nchi hiyo, Donald Trump kuwa anaunga mkono ugaidi wa wazungu dhidi ya wasiokuwa wazungu katika propaganda zake za uchaguzi wa rais.
-
Kukiri Biden kufeli siasa za Trump mbele ya Iran
Sep 15, 2020 02:51Huku wakati wa kufanyika uchaguzi wa Rais wa mwezi Novemba 2020 ukizidi kukabiria nchini Marekani, wagombea wawili wa uchaguzi huo, yaani rais wa hivi sasa Donald Trump na mpinzani wake Joe Biden wa chama cha Democrats kila mmoja amekuwa akitangaza misimamo yake kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo misimamo yao kuhusu Iran na mapatano ya nyuklia ya JCPOA.
-
Sisitizo la Troika ya Ulaya la kutokuwa na itibari jaribio la Marekani la kutaka kurejesha vikwazo dhidi ya Iran
Sep 12, 2020 02:54Baada ya kugonga mwamba hatua za kila aina ilizojaribu kuchukua Marekani ili kurefusha vikwazo vya silaha dhidi ya Iran, Washington iliibua dai la kutaka kurejesha vikwazo vya kimataifa dhidi ya Tehran, ambavyo viliondolewa baada ya kufikiwa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA;
-
Mahakama ya Marekani yataka kusailiwa maafisa wanne wa Saudi Arabia kwa kuhusika na mashambulizi ya Septemba 11
Sep 11, 2020 09:52Baada ya mashambulizi ya Septemba 11 mwaka 2001 Marekani ilijinadi kuwa kinara wa mapambano dhidi ya ugaidi duniani na ikachukua hatua ya kuzivamia nchi za Iraq na Afghanistan.