Pelosi: Timu ya utabibu ya Trump iseme ukweli
https://parstoday.ir/sw/news/world-i63821-pelosi_timu_ya_utabibu_ya_trump_iseme_ukweli
Spika wa bunge la wawakilishi la Marekani amewataka madaktari wanaomhudumia Rais wa nchi hiyo kutoa taarifa sahihi kwa wananchi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 04, 2020 23:27 UTC
  • Pelosi: Timu ya utabibu ya Trump iseme ukweli

Spika wa bunge la wawakilishi la Marekani amewataka madaktari wanaomhudumia Rais wa nchi hiyo kutoa taarifa sahihi kwa wananchi.

Bi Nancy Pelosy amefanya mahojiano na televisheni ya CBS na kuitaka timu ya utabibu ya Trump kutoa taarifa za kuaminika kwa wananchi kuhusu hali ya Rais Trump hivi sasa baada ya kuathiriwa na maambukizi ya corona. 

Pelosy amefanya mahojiano hayo kabla ya timu ya utabibu ya Rais Donald Trump kukutana na waandishi wa habari katika hospitali ya Walter Reed ambako amelazwa. 

Rais Trump amepatwa na corona

Akizungumza na waandishi wa habari jana Sean P. Conley daktari wa White House alieleza kuwa iwapo mchakato wa kupata nafuu Rais Donald Trump utaendelea basi hadi kufikia leo Jumatatu anaweza kuruhusiwa kutoka hospitali. 

Rais wa Marekani Alhamisi iliyopita alilazwa katiak hospitali ya jeshi huko Marekani baada ya kuambukizwa corona baadhi ya washauri na wasaidizi wake na yeye kuonyesha dalili za corona. Trump amelazwa ikiwa umesalia mwezi mmoja tu hadi kufanyika uchaguzi muhimu huko Marekani tarehe tatu mwezi ujao wa Novemba.  

Daktari wa White House, Sean P. Conley juzi alidai kwamba hali ya kiafya ya Trump ni nzuri lakini vyombo vingine vinasema kuwa hali ya kiongozi huyo hairidhishi. Takwimu za kimataifa zinaonyesha kuwa kwa sasa Marekani ndiyo inayoongoza kwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya watu waliopatwa na virusi vya corona na vilevile idadi kubwa zaidi ya watu walioaga dunia kutokana na virusi hivyo.