-
UN: Eritrea imeshindwa kueleza waliko wanasiasa na wanahabari waliotoweka
Mar 30, 2019 03:24Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wamesema serikali ya Eritrea imeshindwa kutoa ufafanuzi kuhusu waliko wanaharakati wa kisiasa na waandishi wa habari waliokamatwa na maafisa usalama au waliotoweka katika mazingira ya kutatanisha nchini humo.
-
Marekani yaendeleza uhasama dhidi ya Iran, mara hii ni kwa kisingizio cha haki za binadamu
Mar 15, 2019 12:58Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imetoa ripoti yake ya kila mwaka kuhusu hali ya haki za binadamu katika nchi mbalimbali na kwa mara nyingine tena imedai kuwa, hali ya haki za binadamu nchini Iran imekuwa mbaya zaidi.
-
Iran: Serikali ya Marekani ndiyo mkiukaji mkubwa kabisa wa haki za binadamu
Mar 15, 2019 03:50Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema: Serikali ya Marekani ndiyo mkiukaji mkubwa kabisa wa haki za binadamu za wananchi wa Iran, kwani kwa kuwatwisha vikwazo vyake haramu vya nje ya mipaka na vya upande mmoja, Washington haijasita kuchukua hatua yoyote ya kukanyaga haki za raia wa Iran.
-
Amnesty International yaitaka Saudia iwaachie huru wanaharakati wa kike
Mar 08, 2019 10:16Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limeitisha maandamano mbele ya ubalozi wa Saudi Arabia mjini Paris huko Ufaransa kulalamikia hatua ya serikali ya Riyadh ya kuendelea kuwashikilia wanaharakati wa kike wa kutetea haki za binadamu.
-
Umoja wa Mataifa: Iran inaongoza kuhusu kuheshimu haki za binaadamu magharibi mwa Asia
Mar 06, 2019 23:24Naibu Kamishna Mkuu wa Haki za Binaadamu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, Iran ni moja ya nchi zinazoongoza kuhusiana na suala la kuheshimiwa haki za binaadamu katika eneo la magharibi mwa Asia na kuongeza kuwa, wanawake wa Iran wako katika mstari wa mbele katika nyanja tofauti.
-
El Baradei akosoa ukandamizaji dhidi ya wafungwa wa kisiasa Misri
Mar 03, 2019 23:10Makamu wa zamani wa rais wa Misri amekosoa ukandamizaji unaofanywa na serikali ya nchi hiyo dhidi ya wafungwa wa kisiasa ikiwa ni pamoja na kuzuia familia za wafungwa hao kuwatembelea korokoroni kwa kipindi kirefu.
-
Amnesty International: Idadi ya wakimbizi wa Kisaudia nje ya nchi inaongezeka
Feb 17, 2019 01:05Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limetangaza kuwa, idadi ya raia wa Saudi Arabia wanaoomba hifadhi na ukimbizi katika nchi mbalimbali duniani inaendelea kuongezeka na kwamba, hiyo ni ishara ya kuporomoka sana uhuru wa kiraia, kijamii na kidini nchini humo.
-
Hali ya haki za binadamu Bahrain ni mbaya sana
Feb 12, 2019 23:02Kamati ya Kimatiafa ya Haki za Binadamu Eneo la Asia Magharibi imesema hali ya haki za binadamu inazidi kuwa mbaya nchini Bahrain ambapo ukoo wa Aal Khalifa ambao unatawala nchi hiyo umehusika na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.
-
HRW: Jeshi la Burkina Faso limewaua watuhumiwa mbele ya familia zao
Feb 06, 2019 11:55Mashiriki ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu yamelituhumu jeshi la serikali ya Burkina Faso kuwa limewaua kinyama watuhumiwa wa vitendo vya kigaidi tena mbele ya watu wa familia zao.
-
Marekani yashindwa kuzuia uteuzi wa Bachelet kuwa Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa UN
Jan 31, 2019 22:51Jarida la Marekani la Foreign Policy limefichua kwamba, kabla ya kuteuliwa Michelle Bachelet kuwa Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Marekani ilifanya jitihada kubwa za kuzuia uteuzi huo lakini jitihada hizo zimeambulia patupu.