-
Afungwa miaka mitano jela kwa kusema tu Wayemen wanaonewa
Dec 31, 2018 13:37Ikiwa ni kuendeleza dhulma yake isiyo na kifani, utawala wa kiimla wa ukoo wa Aal Khalifa wa nchini Bahrain umemuhukumu kifungo cha miaka mitano jela, mwanaharakati maarufu Nabil Rajab kwa kuandika tu katika mtandao wa Twitter kwamba Wayemen wanadhulumiwa na muungano vamizi wa Saudi Arabia.
-
Haki za binadamu, kuanzia nara hadi matendo
Dec 12, 2018 11:07Jumatatu ya tarehe 10 Disemba wiki hii dunia iliadhimisha Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu. Hii leo suala la Haki za binadamu limekuwa miongoni mwa mijadala muhimu zaidi katika fikra za walimwengu na kwenye duru mbalimbali za kimataifa.
-
Uganda nayo yaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu + Sauti
Dec 10, 2018 18:13Uganda imejiunga na nchi nyingine dunia katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Haki za binadamu. Sherehe hiyo imehutubiwa na Rais Yoweri Museveni wa Uganda ambaye ametangaza mkakati mpya wa kupambana na ufisadi ambao umeutaja kuwa ni sawa na maradhi ya saratani. Kigozi Ismail na ripoti kamili...
-
Kenya yaorodheshwa kati ya nchi zisizochunga haki za binadamu kwa raia + Sauti
Dec 10, 2018 18:07Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limeiorodhesha Kenya miongoni mwa mataifa ambayo hayajazingatia kikamilifu haki za raia wake duniani. Ripoti ya shirika hilo iliyozinduliwa leo Jumatatu imeiorodhesha Idara ya Polisi ya Kenya kuwa inaongoza katika ukiukaji wa haki hizo. Mwandishi wetu wa Kenya, Seifullah Murtadhaa anayo maelezo zaidi...
-
Burundi yaiagiza UN ifunge ofisi yake ya haki za binadamu Bujumbura
Dec 06, 2018 14:54Serikali ya Burundi imeliagiza Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa lifunge ofisi yake iliyoko katika mji mkuu wa nchi hiyo, Bujumbura katika kipindi cha miezi miwili ijayo.
-
Mwanahakari ataka kufanywa uchunguzi maalumu katika jela za Saudia
Nov 23, 2018 14:50Kiongozi wa masuala ya Saudi Arabia katika shirika la haki za binaadamu la Human Rights Watch ametaka kufanyike uchunguzi wa kimataifa kuhusiana na hali ya wafungwa nchini humo.
-
Kukosolewa siasa za Saudi Arabia zilizo dhidi ya haki za binadamu
Nov 22, 2018 02:39Shirika la Msamaha Duniani la Amnesty International limekosoa vikali kutiwa mbaroni watu nchini Saudi Arabia na kuteswa wanaharakati wa haki za binadamu katika magereza ya nchi hiyo.
-
UN: Waislamu wa Rohingya wanakabiliwa na hatari kubwa wakirejeshwa Myanmar
Nov 14, 2018 02:39Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa ameitaka serikali ya Bangladesh kusimamisha mpango wake wa kuwarejesha kwa nguvu nchini Myanmar maelfu ya wakimbizi Waislamu wa Rohingya akisisitiza kuwa maisha yao yatakuwa hatarini.
-
AI: Kadhia ya Khashoggi imedhihirisha unafiki wa Wamagharibi kuhusu Saudia
Nov 03, 2018 14:39Msemaji wa shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International amesema kuwa mauaji ya kikatili ya mkosoaji wa utawala wa Saudi Arabia, Jamal Khashoggi yamedhihirisha wazi unafiki wa Ulaya na Marekani kuhusiana na haki za binadamu nchini Saudi Arabia.
-
Kadhia ya mauaji ya Jamal Khashoggi yajadiliwa katika kikao cha haki za binaadamu mjini Paris
Oct 31, 2018 02:27Kadhia ya mauaji ya Jamal Khashoggi, mwandishi wa habari mkoasoaji wa utawala wa Saudi Arabia, imepewa uzingatiaji na kikao cha dunia cha haki za binaadamu mjini Paris, Ufaransa.