Nov 23, 2018 14:50 UTC
  • Mwanahakari ataka kufanywa uchunguzi maalumu katika jela za Saudia

Kiongozi wa masuala ya Saudi Arabia katika shirika la haki za binaadamu la Human Rights Watch ametaka kufanyike uchunguzi wa kimataifa kuhusiana na hali ya wafungwa nchini humo.

Amani al-Ahmadi, mkuu wa masuala ya Saudi Arabia katika kituo cha shirika la Human Rights Watch cha Ulaya na Mediterranean amesema hayo akielezea wasi wasi wake kutokana na jinai zinazofanywa na Riyadh dhidi ya wafungwa ndani ya jela zake.

Ameongeza kwamba, ni lazima uchunguzi wa kimataifa kuhusiana na jinai za jela za Saudia, ufanyike kama lilivyo suala la mauaji ya Jamal Khashoggi, mwandishi wa habari na mkosoaji wa utawala wa Aal-Saud.

Sehemu ya mrundikano wa wafungwa ndani ya jela za Saudia

Kwa mujibu wa kiongozi huyo wa masuala ya haki za binaadamu wa Human Rights Watch, Saudi Arabia ina kesi nyingi za ukiukaji mkubwa wa haki za binaadamu. Hiba Zayadin, mtafiti wa shirika la haki za binadamu la Human Rights Watch amesema kuwa, baadhi ya wanaharakati wa kike wanaoshikiliwa katika jela za Saudia, wamekuwa wakiteswa kwa kutumia umeme au kupigwa mijeledi huku wengine wakinajisiwa na maafisa wa serikali ya nchi hiyo. Hiba Zayadin ameongeza kwamba baadhi ya wanawake hao wanashikiliwa katika jela za Saudi Arabia kwa muda mrefu na hawajawahi kufikishwa mahakamani hadi sasa.

Tags