Jan 08, 2019 07:36 UTC
  • UNODC: Idadi ya waathirika wa magendo ya binadamu imeongezeka

Idadi ya waathirika wa usafirishaji haramu wa binadamu imeongezeka, huku idadi ya makundi yaliyojizatiti kwa silaha na magaidi yakiendelea kusafirisha wanawake na watoto kwa ajili ya kupata fedha na kuwaandikisha kama wafuasi.

Hayo ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupambamba na Dawa za Kulevya na Uhalifu, ambayo imetangazwa rasmi Jumatatu mjini Vienna Austria. 

Akiwasilisha ripoti hiyo ambayo imetathmini nchi 142 kuhusu mienendo ya usafirishaji haramu wa binadamu na uhalifu huo katika maeneo ya mizozo ya silaha, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupambamba na Dawa za Kulevya na Uhalifu, UNODC , Yury Fedeotov amesema, “watoto wanaotumikishwa jeshini, kazi za lazima, utumwa wa kingono na usafirishwaji haramu umechukua sura mpya na ya kusikitisha wakati vikundi vilivyojizatiti kwa silaha na magaidi vikisambaza hofu na kutumia vishawishi ili kuwapata wafuasi wapya.”

Fedotov amesema ripoti imeonesha wazi kuwa, kuna haja ya kuimarisha misaada yaw kiufundi na ushirikiano, kusaidia nchi mbalimbali kwa ajili ya kulinda manusura wake na kuwawajibisha wahalifu mbele ya sheria ili kufikia malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.

Wahajiri waafrika wakielekea Ulaya

Akizungumza katika hafla hiyo maalumu ya kamisheni ya kuzuia uhalifu na uhalifu wa kisheria wakati wa uzinduzi huo, Waziri wa Maswala ya Kigeni wa Austria, Karin Kneissl, ametaja umuhimu wa ripoti kuangazia msaada kwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa katika kukabiliana na ukikwaji mkubwa wa haki za binadamu. 

Aidha ripoti imebaini kuwa kuna ongezeko la watoto wanaosafirishwa kwa njia haramu ikiwa ni asilimia 30 ya visa vyote huku wasichana wengi wakiathirika zaidi ikilinganishwa na wavulana. Ukatili wa kingono ndio kichocheo kikubwa cha usafirishaji haramu ikijumuisha asilimia 59 ya visa vyote.

Tags