-
Iran yalaani jaribio la mauaji dhidi ya Rais wa Zimbabwe
Jun 24, 2018 03:03Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani vikali jaribio lililofeli la mauaji dhidi ya Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa katika mji wa Bulawayo jana Jumamosi.
-
Sera za Marekani zimepelekea kuendelea migogoro katika eneo
Jun 23, 2018 20:44Mwenyekiti wa Tume ya Usalama wa Taifa na Sera za Kigeni katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, Bunge la Iran, amesema: Sera za kivita na za kuunga mkono makundi ya kigaidi zinazotekelezwa na Marekani sambamba na hatua ya nchi hiyo kukiuka mikataba ya kimataifa hasa mapatano ya nyuklia ya Iran, JCPOA, ni chazo cha kuendelea migogoro katika eneo."
-
ICJ kusikiliza kesi ya Iran dhidi ya Marekani kuhusu uzuiaji mabilioni ya dola
Jun 23, 2018 09:23Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu (ICJ) imesema itasikiliza kesi iliyowasilishwa na Iran dhidi ya Marekani kuhusu mabilioni ya dola ya fedha za Iran ambazo serikali ya Marekani imezuzuia katika benki za nchi hiyo.
-
Araqchi: JCPOA ipo katika ICU, yumkini Iran ikajiondoa wiki chache zijazo
Jun 23, 2018 02:51Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na masuala ya kisiasa amesema makubaliano ya nyuklia kati ya Iran na nchi sita za kundi la 5+1 maarufu kama JCPOA yako chumba cha wagonjwa mahututi ICU, na yumkini Tehran ikajiondoa kwenye mapatano hayo ndani ya wiki chache zijazo.
-
Jumamosi, Juni 23, 2018
Jun 22, 2018 21:50Leo ni Jumamosi tarehe 10 Shawwal, mwaka 1439 Hijria, inayosadifiana na tarehe 23 Juni mwaka 2018 Miladia.
-
Rouhani: Wairani hawawezi kupigishwa magoti na njama za Marekani
Jun 21, 2018 09:43Rais Hassan Rouhani amesema katu taifa la Iran haliwezi kupigishwa magoti na njama na mashinikizo ya dola la kibeberu la Marekani.
-
Mabaharia 17 wa Kiirani waliokamatwa Somalia waachiwa huru
Jun 21, 2018 09:11Mabaharia 17 wa Kiirani waliokuwa wameingia kimakosa katika maji ya Somalia na kutiwa nguvuni mwishoni mwa mwaka jana 2017 wameachiwa huru na kurejea nchini.
-
Utambulisho halisi wa Marekani kwa mtazamo wa Kiongozi Muadhamu
Jun 21, 2018 02:40Kingozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei, Jumatano asubuhi alikutana na Spika wa Majlisi ya Kiislamu, Bunge la Iran, wabunge na wafanyakazi wa bunge ambapo alibainisha utambulisho na malengo halisi ya Marekani katika eneo.
-
Zarif: Sera za kigeni za Marekani zimekumbwa na mgogoro
Jun 20, 2018 23:14Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran katika makala yenye anwani inayosema: "Sera za Kigeni za Marekani Katika Mgogoro" ameandika: "Mapatano ya nyuklia ya Iran (JCPOA) yalikuwa mapatano ya tatu ya kimataifa Marekani kujiondoa baada ya kujiondoa katika mapatano ya kibiashara ya Bahari ya Pasifiki na mapatano ya tabianchi ya Paris."
-
IRGC: Iran ipo tayari kukabiliana na ugaidi wa kibiolojia
Jun 20, 2018 03:16Kamanda wa ngazi za juu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) ameashiria hatua zilizochukuliwa na Sepah kwa ajili ya kuzima jaribio lolote la shambulizi la kibiolojia na kusema kwamba, kitengo cha usalama cha jeshi hilo kimekuwa kikitoa mafunzo sambamba na kuzalisha zana za kukabiliana na ugaidi wa kibiolojia.