Mabaharia 17 wa Kiirani waliokamatwa Somalia waachiwa huru
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i46138-mabaharia_17_wa_kiirani_waliokamatwa_somalia_waachiwa_huru
Mabaharia 17 wa Kiirani waliokuwa wameingia kimakosa katika maji ya Somalia na kutiwa nguvuni mwishoni mwa mwaka jana 2017 wameachiwa huru na kurejea nchini.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 21, 2018 09:11 UTC
  • Mabaharia 17 wa Kiirani waliokamatwa Somalia waachiwa huru

Mabaharia 17 wa Kiirani waliokuwa wameingia kimakosa katika maji ya Somalia na kutiwa nguvuni mwishoni mwa mwaka jana 2017 wameachiwa huru na kurejea nchini.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, mabaharia hao wameachiwa huru kutokana na jitihada za kidiplomasia za Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran na ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu mjini Nairobi, Kenya.

Mabaharia hao wanadaiwa kuingia kimakosa katika maji ya Somalia mnamo Oktoba mwaka jana, ambapo walikamatwa na kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela kila mmoja mbali na kutozwa faini.

Kisiwa cha Kismayo nchini Somalia

Mabaharia hao wa Kiirani wamewasili hapa nchini leo Alkhamisi na kupokewa katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Imam Khomeini hapa mjini Tehran na Hossein Panahi Azar, Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Itakumbukwa kuwa, Februari mwaka jana, mabaharia wengine 8 raia wa Iran walioingia kimakosa katika maji ya Tanzania na kukamatwa na jeshi la nchi hiyo waliachiwa huru baada ya ufuatiliaji uliofanywa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran kuhusu maudhui hiyo.