-
Jumatano, Juni 21, 2017
Jun 20, 2017 22:13Leo ni Jumatano tarehe 26 Ramadhani, 1438 Hijria, sawa na Juni 21, 2017.
-
Kiongozi Muadhamu: Iran inapinga kura ya maoni ya kujitenga eneo moja la Iraq
Jun 20, 2017 12:42Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyed Ali Khamenei amepongeza umoja na mshikamano wa makundi yote ya kisiasa na kimadhehebu Iraq katika mapambano dhidi ya ISIS au Daesh na kusema uwepo wa 'Vikosi vya Kujitolea vya Wananchi' ni tuko muhimu na lenye baraka ambalo ni chanzo cha nguvu nchini Iraq.
-
Zarif: Hakuna kizuizi cha kuimarisha uhusiano wa Iran na Tunisia
Jun 20, 2017 03:28Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema hakuna kitu kinachoweza kuzuia au kukwamisha kuimarisha uhusiano wa pande mbili wa Iran na Tunisia.
-
Kichapo cha makombora ya Iran kwa magaidi wa Daesh (ISIS) katika eneo la Deir Ezzor, Syria
Jun 20, 2017 01:49Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) Jumapili usiku lilishambulia kwa makombora sita ya masafa ya kati ya ardhini kwa ardhini kamandi ya kijeshi ya magaidi wa kitakfiri wa Daesh (ISIS) katika eneo la Deir Ezzor mashariki mwa Syria.
-
Trump na vitisho dhidi ya Iran kwa mtazamo wa Kiongozi Muadhamu
Jun 19, 2017 08:10Ayatullah Sayyed Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu jana Jumapili alikutana mjini Tehran na familia za mashahidi walinzi wa Haram Takatifu na vikosi vya usalama vinavyolinda mipaka ya nchi na kusisitiza umuhimu wa mashahidi katika uhai wa Iran.
-
Brigedia Jenerali Jazayeri: Iran ina njia ya kuiadhibu Marekani
Jun 18, 2017 23:08Naibu Mkuu wa Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Tehran ina namna na njia ya kuiadhibu Washington baada ya Bunge la Seneti la Marekani kupasisha vikwazo vipya dhidi ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran IRGC kwa madai yasiyo na msingi ya ugaidi.
-
Safari ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran barani Afrika
Jun 17, 2017 23:22Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo (Jumapili) anaanza ziara ya kuzitembelea nchi za Algeria, Mauritania na Tunisia.
-
Zarif: Marekani badala ya kufikiria kubadilisha mfumo wa Iran ifikirie kulinda utawala wake
Jun 16, 2017 03:13Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Iran ameitaka Marekani ifikirie namna ya kulinda utawala wake badala ya kuhangaika ikitaka kubadilisha mfumo unaotawala nchini Iran.
-
Matamshi ya uingiliaji ya Tillerson; kilele cha kuchanganyikiwa Marekani mbele ya Iran
Jun 16, 2017 02:51Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani ameonyesha msimamo ambao ni wa uhasama na uingiliaji wa moja kwa moja katika masuala ya ndani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambayo hivi sasa inaelekea kutimiza miaka arubaini ya uhai wake.
-
Vaezi: Iran iko tayari kutoa huduma za teknolojia ya mawasiliano barani Afrika
Jun 15, 2017 11:00Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia wa Iran amekutana na mawaziri wa nchi za Kiafrika mjini Geneva na kusema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu iko tayari kutoa huduma za kiufundi na kihandisi katika sekta ya teknolojia ya mawasiliano kwenye nchi mbalimbali za Afrika.