-
Onyo la Iran kwa waungaji mkono wa Israel; Kaeni mbali na vita
Oct 04, 2024 04:22Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amezionya nchi za Magharibi na waungaji mkono wengine wa Israel katika eneo dhidi ya kuingilia mzozo kati ya Jamhuri ya Kiislamu na utawala wa Kizayuni.
-
Israel yaendelea kumwaga damu za Walebanon mjini Beirut
Oct 04, 2024 03:43Wizara ya Afya ya Lebanon imesema takriban watu 37 wameuawa shahidi huku wengine zaidi ya 150 wakijeruhiwa katika mashambulizi mapya ya anga ya utawala haramu wa Israel, huku uchokozi usio na kikomo wa utawala huo katili dhidi ya Lebanon ukiendelea.
-
Kikao cha Baraza la Usalama la UN na makabiliano ya mitazamo kuhusu matukio ya eneo la Asia Magharibi
Oct 03, 2024 07:46Kikao cha dharura cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kilichoitishwa kujadili matukio ya Asia Magharibi kufuatia shambulio la makombora lililofanywa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kujibu jinai za Israel kimeambatana na matamshi ya kifidhuli yaliyotolewa na mwakilishi wa utawala huo wa Kizayuni ukiungwa mkono na nchi za Magharibi.
-
Tathmini ya vipengele vya kijeshi vya Operesheni ya Ahadi ya Kweli -2: Jibu kwa shari za Israeli
Oct 02, 2024 07:44Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) jana usiku lilitoa taarifa likitangaza kuwa limeshambulia kitovu cha maeneo yanayokaliwa kwa mabavu ya Palestina (Israel) ikiwa ni katika kujibu mauaji ya shahidi Ismail Haniyeh, Sayyid Hassan Nasrullah na Meja Jenerali Abbas Nilforoushan Kamanda na mshauri wa ngazi ya juu wa IRGC huko Lebanon.
-
Iran yauandikia barua muhimu Umoja wa Mataifa na kutoa onyo kali kwa utawala wa Kizayuni wa Israel
Oct 02, 2024 05:37Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amemwandikia barua Katibu Mkuu na Rais wa Baraza la Usalama la umoja huo kufuatia operesheni ya makombora iliyofanywa na Iran, na kusisitiza kuwa, endapo utawala wa Israel utarudia tena vitendo vyake vinavyokiuka sheria za kimataifa, jibu litakalotolewa tena na Iran litakuwa la haraka, madhubiti na kali zaidi kuliko lililiotangulia.
-
HAMAS: Tumeangamiza idadi kubwa ya askari wa Israel Gaza
Sep 30, 2024 23:49Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imetangaza habari ya kuangamiza idadi kubwa ya wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel kusini mwa Ukanda wa Gaza.
-
Madai ya Marekani katika muktadha wa kujaribu kuzuia vita Asia Magharibi
Sep 30, 2024 22:47Marekani ambayo ni mdhamini mkubwa zaidi wa silaha kwa utawala wa Kizayuni wa Israel kwa ajili ya mashambulizi makubwa dhidi ya watu wa Lebanon na Gaza, sasa inajitokeza kwa unafiki na kutoa wito wa kupunguzwa mivutano na kurejeshwa amani katika eneo la Magharibi mwa Asia.
-
Hizbullah yaipiga kambi ya kijeshi ya Israel kwa makombora ya Fadi-1
Sep 29, 2024 22:57Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon imesema imevurumisha makombora ya Fadi-1 dhidi ya kambi ya jeshi la Israel katika maeneo ya kaskazini yanayokaliwa kwa mabavu.
-
Hamas: Kuuawa makamanda wa Hizbullah hakuifanyi Israeli kuwa salama zaidi
Sep 28, 2024 22:47Kufuatia mashambulizi ya kikatili ya utawala wa Kizayuni wa Israel huko Beirut, Hamas imeonya kuwa, hatua hizo hazitaifanya Israel kuwa sehemu salama zaidi.
-
Guardian: Shambulio lolote la ardhini litakalofanywa na Israel dhidi ya Lebanon litafeli
Sep 28, 2024 07:50Gazeti la Guardian la Uingereza limeandika kuwa operesheni yoyote ya ardhini itakayofanywa na utawala wa Israel dhidi ya Lebanon itafeli na kugonga mwamba.