-
UK, Ufaransa na Ujerumani zaonywa kwa kutuma ndege kuilinda Israel katika Operesheni ya Ahadi ya Kweli
May 16, 2024 03:55Brigedia Jenerali Esmail Qa’ani, Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ametoa onyo kwa Uingereza, Ujerumani na Ufaransa baada ya nchi hizo tatu za Troika ya Ulaya kupeleka ndege zao za kivita kuulinda utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya operesheni ya kulipiza kisasi ya Ahadi ya Kweli iliyofanywa na Iran mwezi uliopita wa Aprili.
-
Marekani kukanusha tena kutokea mauaji ya kimbari huko Ukanda wa Gaza, ni kukana ukweli ulio wazi
May 16, 2024 00:55Licha ya Wapalestina zaidi ya elfu 35,000 kuuawa shahidi na utawala wa kigaidi wa Israel huko Ukanda wa Gaza, lakini Jake Sullivan, Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Ikulu ya White House nchini Marekani amedai bila kuona haya kwamba serikali ya Rais Joe Biden haiyachukulii mauaji hayo kuwa ni mauaji ya halaiki.
-
"Mauaji ya watoto 15,000 wa Gaza yanaashiria mwisho wa Israel"
May 14, 2024 23:49Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema hakuna shaka kuwa mauaji ya watoto zaidi ya 15,000 wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza itakuwa chachu ya kuharakisha mchakato wa kuporomoka na kusambaratika utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Iran: Israel ni nembo ya ugaidi ulioratibiwa duniani
May 14, 2024 08:27Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imeutaja utawala wa Kizayuni wa Israel kama nembo kuu ya ugaidi ulioratibiwa duniani.
-
Makumi ya Wapalestina wauawa katika hujuma za Israel Gaza
May 14, 2024 07:35Ndege za kivita za utawala wa Kizayuni wa Israel zimefanya mashambulizi mapya ya anga dhidi ya maeneo tofauti ya Ukanda wa Gaza na kuua shahidi makumi ya Wapalestina, wakiwemo watoto wadogo na wanawake.
-
Jumanne, tarehe 14 Mei, 2024
May 14, 2024 00:09Leo ni Jumanne tarehe 5 Dhulqaada 1445 Hijria sawa na tarehe 14 Mei 2024.
-
Uingereza yatupilia mbali miito ya kuitaka isitishe uuzaji silaha kwa Israel
May 13, 2024 00:35Serikali ya Uingereza imekataa miito ya kuitaka ifuate mwelekeo ulioonyeshwa na Marekani wa kutishia kusitisha baadhi ya mauzo ya silaha kwa utawala wa Kizayuni wa Israel ikiwa utafanya operesheni kubwa ya ardhini katika mji wa Rafah kusini mwa Ukanda wa Ghaza unaowapa hifadhi wakimbizi Wapalestina wapatao milioni moja na laki nne.
-
Iran: Israel haijawahi kutengwa kiasi hiki katika historia yake bandia
May 11, 2024 23:40Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameashiria hatua ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA ya kupasisha rasimu ya azimio la kutaka kutazamwa upya suala la taifa la Palestina kupewa uanachama kamili katika umoja huo na kusema kuwa, utawala haramu wa Israel haujawahi kutengwa kwa kiwango kikubwa kama cha sasa katika historia yake bandia.
-
Afisa wa Hamas: Muqawama wa Gaza umeweza kukabiliana kwa mafanikio na vita vya dunia
May 11, 2024 23:06Sami Abu Zuhri, ambaye ni miongoni mwa viongozi wa ngazi za juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS), amesema kwamba Muqawama na mapambano ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza yamefanikiwa kukabiliana na "vita vya kimataifa," na nchi zilizoifadhili Israel sasa zinaanza kusitisha uungaji mkono wao kwa utawala huo.
-
Iran: Kuipa uanachama Palestina, ni hatua ya kwanza ya kukabiliana na dhulma
May 11, 2024 04:31Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema Tehran inakaribisha hatua ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA ya kupasisha azimio la kutaka kutazamwa upya suala la taifa la Palestina kupewa uanachama kamili katika umoja huo.