-
Ugonjwa 'usiojulikana' waua makumi ya watu DRC; mapigano yanaendelea
Feb 14, 2025 12:10Ugonjwa usiojulikana umeua watu zaidi ya 50 katika eneo la Bansakusu, jimbo la Equateur, magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
UN: Maelfu ya raia Kongo wahama makazi yao baada ya M23 kutoa muhula wa masaa 72
Feb 12, 2025 09:20Waasi wa M23 wanaodhibiti miji ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamefunga kwa nguvu kambi za makazi za raia na kuwalazimisha zaidi ya watu 110,000 kuhama makazi yao katika siku za hivi karibuni. Haya yameelezwa na Umoja wa Mataifa.
-
Bunge la Afrika Mashariki lasimamisha vikao vyake kwa muda usiojulikana kwa sababu za kifedha
Feb 10, 2025 07:00Bunge la nchi za Afrika Mashariki, EALA limetangaza kuwa limesimamisha vikao vyake kwa muda usiojulikana kutokana na changamoto za kifedha, zilizosababishwa na baadhi ya nchi wanachama kushindwa kulipa michango yao ya fedha.
-
Jumuiya za SADC na EAC zataka kusitishwa mapigano Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Feb 09, 2025 03:25Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na ile ya nchi za kusini mwa Afrika, SADC wametoa mwito wa kusitishwa mara moja mapigano mashariki mwa Jamhuuri ya Kidemokkrasia ya Congo.
-
Maafisa wa SADC na EAC watilia mkazo kusitishwa mapigano mashariki mwa Kongo
Feb 08, 2025 07:49Maafisa wa ngazi ya juu kutoka mataifa ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika jana walitilia mkazo kusitishwa mara moja mapigano mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kuzitaka pande zote husika kutoa kipaumbele kwa suala la kufanya mazungumzo ili kuupatia ufumbuzi mgogoro uliopo.
-
UN: Hali ya kibinadamu huko Goma bado ni mbaya licha ya kusimamishwa mapigano
Feb 07, 2025 02:39Hospitali katika mji mkubwa wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Goma, zinatatizika kutibu mamia ya wagonjwa waliojeruhiwa, huku baadhi wakiripoti uhaba wa dawa siku chache baada ya kundi la waasi la M23 kutangaza kusitisha mapigano kwa upande mmoja.
-
Mahakama ya Kijeshi ya DRC yatoa hati ya kukamatwa Corneille Nangaa
Feb 06, 2025 11:17Mahakama ya Kijeshi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imetoa hati ya kukamatwa kwa Corneille Nangaa, mkuu wa makundi ya waasi wa mashariki mwa nchi hiyo, ikimtuhumu kwa kushindwa kuzuia vitendo vya utesaji chini ya mamlaka yake.
-
Uganda yatuma askari 1,000 zaidi mashariki mwa DRC
Feb 05, 2025 02:40Uganda imeripotiwa kutuma wanajeshi zaidi ya 1,000 wa ziada huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ndani ya wiki moja iliyopita, karibu na eneo ambalo wanajeshi wa serikali ya Kinshasa wanapambana na waasi wa M23.
-
Muungano wa waasi wa mashariki mwa Kongo likiwemo kundi la M23 watangaza kusitisha mapigano
Feb 04, 2025 07:30Muungano kwa jina la The Alliance Fleuve Congo; muungano wa waasi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo unaolijumuisha pia kundi la waasi wa M23 umetangaza kusitisha mapigano kuanzia leo Jumanne Februari 4.
-
Utulivu wa kulegalega washuhudiwa Goma; Mapigano yapungua mashariki mwa DRC
Feb 02, 2025 07:45Ripoti mbalimbali zinaeleza kuwa licha ya kurejea utulivu wa kiwango fulani katika mji wa Goma, makao makuu ya jimbo la Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, mashirika ya misaada ya kibinadamu yameonya juu ya kushtadi hali ya mambo huku hospitali zikizidiwa na wagonjwa, uhaba wa vifaa muhimu vya tiba ukishuhudiwa na miili ya watu waliouawa ikiendelea kuonekana mitaani.