Waasi wa ADF wauwa raia zaidi ya 80 mashariki mwa Kongo
-
Waasi wa ADF
Waasi wanaoshukiwa kuwa wa kundi la Allied Democratic Forces (ADF) wameripotiwa kufanya mauaji ya takriban raia 87 katika mashambulizi tofauti katika vijiji vya mkoa wa Ituri mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imeeleza katika ripoti yake ya kila mwezi kuwa mashambulizi katika eneo la Mambasa yameathiri zaidi maeneo ya afya ya Nia-nia na Lolwa.
Mbali na maafa hayo, mashambulizi ya waasi wa ADF yamewalazimisha raia zaidi ya 60,000 kuhama makazi yao na kuelekea katika maeneo mengine salama huko Mambasa na katika jimbo jirani la Tshopo.
Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limesema kuwa hatua za usalama zimetekelezwa tangu wakati huo, kuwezesha uokoaji wa mateka wapatao 200 wakati wa operesheni za mapigano zilizofanywa na wanajeshi wa Kongo na Uganda mapema mwezi huu.
Maafisa wanne wa ADF waliuawa wakati wa mashambulizi, akiwemo daktari binafsi wa kiongozi wa kundi hilo, Moussa Bakulu", imeeleza taarifa ya jeshi la Kongo.