-
Bosco Ntangada wa DRC akiwa ICC: Mimi si mhalifu ni mwanamapinduzi
Aug 31, 2018 02:03Mbabe wa zamani wa kivita wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Bosco Ntanganda, amedai mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC, kuwa yeye si mhalifu bali ni mwanamapinduzi.
-
Waasi wa ADF- Nalu washambulia jeshi la Kongo mashariki mwa nchi
Aug 26, 2018 03:02Duru za kijeshi na za kiraia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zimeetangaza kuwa waasi wa Uganda kwa jina la ADF- Nalu wameshambulia kitengo kimoja cha vikosi vya jeshi la Kongo mashariki mwa nchi hiyo.
-
SAUTI, Viongozi wa upinzani Kongo DR walaani panga lililokata majina yao kushiriki uchaguzi ujao
Aug 25, 2018 10:15Viongozi wa vyama vya upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wameijia juu Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo (CENI) kwa hatua yake ya kukata majina sita miongoni mwa majina ya waliojiandikisha kugombea kiti cha urais katika uchaguzi ujao nchini humo.
-
Tume ya Uchaguzi DRC yamzuia Bemba kugombea urais
Aug 25, 2018 02:15Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (CENI) imemzuia mpinzani Jean-Pierre Bemba kugombea urais katika uchaguzi ujao wa rais.
-
WHO: Mlipuko wa Ebola DRC umeshadhibitiwa lakini hatari bado ipo
Aug 24, 2018 21:51Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema mlipuko mpya wa ugonjwa wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) umeshadhibitiwa, lakini kuna uwezekano wa kutokea kesi mpya, kutokana na mazingira magumu yanayosababishwa na hali mbaya ya usalama na baadhi ya maeneo kutofikika.
-
Wapinzani waitisha maandamano ya nchi nzima DRC
Aug 22, 2018 09:56Wapinzani wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanataka kusitumike mashine za kupigia kura katika uchaguzi ujao.
-
Spika wa Seneti ya Kongo DR ataka kiongozi wa upinzani aruhusiwe kurudi nchini
Aug 21, 2018 10:50Spika wa Seneti ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ametaka Moïse Katumbi, kiongozi wa upinzani na mmoja wa wapinzani wakuu wa rais wa nchi hiyo Joseph Kabila aruhusiwe kurudi nchini.
-
Idadi ya wahanga wa homa ya Ebola yaongezeka DRC
Aug 21, 2018 03:10Wizara ya Afya ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ilitangaza jana kwamba idadi ya wahanga wa wimbi jipya la kuenea ugonjwa wa Ebola nchini humo imeongezeka na kufikia watu 50.
-
Athari za Ebola kwa watoto DRC ni zaidi ya kuugua –UNICEF
Aug 18, 2018 02:56Watoto wanawakilisha idadi kubwa isiyo ya kawaida ya waathirika wa mlipuko wa Ebola huko mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC, limesema shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF.
-
Waasi wa ADF-NALU wa Uganda wafanya mashambulio DRC na kuua watu 6
Aug 12, 2018 08:29Waasi wa ADF-Nalu wa Uganda wamefanya mashambulio katika jimbo la Kivu Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kuua watu sita.