EU kuwarejeshea vikwazo maafisa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i49162-eu_kuwarejeshea_vikwazo_maafisa_wa_jamhuri_ya_kidemokrasia_ya_kongo
Umoja wa Ulaya unajiandaa kuwarejeshea vikwazo maafisa wa ngazi ya juu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo akiwemo mgombea wa kiti cha urais Emmanuel Ramazani Shadary ifikapo mwezi Disemba mwaka huu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 31, 2018 12:21 UTC
  • EU kuwarejeshea vikwazo maafisa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Umoja wa Ulaya unajiandaa kuwarejeshea vikwazo maafisa wa ngazi ya juu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo akiwemo mgombea wa kiti cha urais Emmanuel Ramazani Shadary ifikapo mwezi Disemba mwaka huu.

Umoja wa Ulaya mwaka jana ulimwekea Shadary vikwazo wakati akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani pamoja na maafisa 15 wa Kongo baada ya askari usalama kukandamiza maandamano ya wapinzani waliokuwa wakipinga kuakhirishwa uchaguzi wa rais. Hatua ya kuakhirisha uchaguzi huo imempelekea Rais Joseph Kabila kusalia madarakani kwa muda wa miaka miwili licha ya muhula wake wa kisheria kumalizika ingawa uchaguzi huo sasa umepangwa kufanyika Disemba 23 mwaka huu. 

Emmanuel Ramazani Shadary, mgombea wa kiti cha urais Kongo

Serikali ya Kinshasa imesema kuwa vikwazo hivyo vya Umoja wa Ulaya ambavyo vinajumuisha marufuku ya kusafiri na uzuiaji wa mali ni kinyume cha sheria na kwamba kitendo cha kurejesha vikwazo hivyo hakina maana kwa sababu Rais Kabila anajiandaa kuondoka madarakani baada ya uchaguzi. Ramazani Shadary anatajwa kuwa chaguo la Joseph Kabila ambaye ndiye aliyeongoza ukandamizaji wa polisi dhidi ya waandamanaji waliokuwa wakipinga hatua ya Rais Kabila ya kuendelea kubakia madarakani. Raia kadhaa waliuliwa na askari usalama kwenye ukandamizaji huo.