Nov 02, 2018 06:02 UTC
  • Wasiwasi wa WHO kuhusu ongezeko la maambukizi mapya ya Ebola DRC

Shirika la Afya Duniani WHO limeeleza wasiwasi wake kuhusu kuongezeka kwa maambukizi ya Ebola yaliyothibitishwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC katika wiki nne zilizopita.

WHO inasema maambukizi hayo yanajiri pamoja na kuwa kumepatikana maendeleo makubwa katika hatua za kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huo.

WHO imesema mengi ya maambukizi mapya yapo katika mji wa Beni na pia maeneo ya Butembo, mkoa wa Kivu Kaskazini, huko kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya  Kongo. WHO imesema ukosefu wa usalama umeendelea  kuwaathiri vibaya raia na wafanyakazi walioko mstari wa mbele wa maeneo yaliyokumbwa na Ebola.

WHO inasema hadi tarehe 23 mwezi wa Oktoba watu 124 walikuwa wamefariki dunia kutokanana Ebola jimboni Kivu Kaskazini na Ituri kufuatia mlipuko mpya wa ugonjwa huo ulioanza Agosti.

Hatari ya mlipuko wa ugonjwa huo kusambaa katika maeneo mengine ya DRC na pia katika nchi zilizoko jirani bado ni kubwa kwa mujibu wa shirika la afya duniani.

Kutokana na mlipuko wa ugonjwa huu wa juma lililopita, tahadhari zimtolewa katika nchi za Mauritania, Sudan Kusini, Sudan, Uganda na Tanzania.

 

Tags