-
Kharrazi amjibu Trump na kumtaka kwanza atekeleze ahadi za serikali zilizotangulia za Marekani
Jul 31, 2018 10:40Mkuu wa Baraza la Kistratijia la Sera za Kigeni la Iran Dkt. Kammal Kharrazi ametoa jibu kwa pandekezo la Rais Donald Trump wa Marekani la kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na wakuu wa Iran na kusema: "Kabla ya yote, Donald Trump anapaswa kutekeleza ahadi na mikataba ya serikali zilizotangulia za Marekani na aheshimu sheria za kimataifa."
-
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran: Serikali ya sasa ya Marekani haiaminiki
Jul 30, 2018 09:56Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema haiwezekani kufanya mazungumzo ya aina yoyote na serikali ya sasa ya Marekani na kusisitiza kuwa serikali ya nchi hiyo haiaminiki.
-
Austria yaikosoa vikali Marekani kutokana na kujiondoa katika JCPOA
Jul 29, 2018 02:56Kujiondoa Marekani katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA Mei mwaka huu, hatua ambayo ilichukuliwa na Rais Donald Trump wa nchi hiyo, kulifuatiwa na ukosoaji mkubwa wa nchi zingine wanachama wa kundi la 5+1 zikiwemo nchi tatu za Troika ya Ulaya za Ufaransa, Uingereza na Ujerumani.
-
Madai ya Donald Trump ya kuwa tayari kufikia makubaliano na Iran
Jul 25, 2018 03:48Licha ya kuweko uadui na uhasama wa Marekani dhidi ya Iran katika kipindi cha miaka takribani 40 tangu kuasisiwa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu, lakini katika kipindi cha uongozi wa Rais Donald Trump, uadui huo ulishadidi zaidi iwe ni katika kipindi cha kampeni za uchaguzi na hata baada ya kuingia madarakani.
-
Kulegeza kamba White House kuhusiana na bwabwaja za Donald Trump dhidi ya Iran
Jul 24, 2018 20:49Katika kipindi cha uongozi wa Rais Donald Trump, Marekani imeshadidisha misimamo na hatua zilizo dhidi ya Iran.
-
Iran yaitaka EU iache maneneo matupu na kutekeleza ahadi kivitendo
Jul 18, 2018 08:34Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran sambamba na kusisitiza umuhimu wa uhusiano wa Iran na Umoja wa Ulaya baada ya Marekani kujiondoa katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA, amesema, baada ya Ulaya kuahidi kufungamana na JCPOA, sasa umewadia wakati wa kutekeleza ahadi hizo kivitendo.
-
AEOI: Iran ipo tayari kuimarisha urutubishaji urani JCPOA ikifeli
Jul 18, 2018 02:56Behrouz Kamalvandi, Msemaji wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (AEOI) amesema Tehran iko tayari kuimarisha urutubishaji urani kwa kiwango cha juu iwapo jitihada za Umoja wa Ulaya za kuyanasuru makubaliano ya nyuklia ya Iran zitagonga mwamba.
-
Kamal Kharrazi: Ulimwengu usimame na kukabiliana na ubeberu wa Marekani
Jul 15, 2018 23:08Mkuu wa Baraza la Kistratijia la Uhusiano wa Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, vikwazo vya Marekani dhidi ya taifa hili ni vya kidhulma na kuongeza kwamba, jamii ya kimataifa inapaswa kusimama kidete na kukabiliana na vikwazo hivyo.
-
Zarif: JCPOA imethibitisha Marekani haiaminiki hata kidogo
Jul 14, 2018 23:27Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran akizungumza kwa munasaba wa kufikiwa mapatano ya nyuklia maarufu kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji, JCPOA, baina ya Iran madola sita makubwa ya kundi la 5+1 amesema: 'JCPOA imethibitisha kuwa serikali ya Marekani haiwezi kuaminika hata kidogo."
-
Rais Rouhani amtumia ujumbe mwenzake wa Uganda, Yoweri Museveni
Jul 12, 2018 10:31Mjumbe maalumu wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amemkabidhi Rais Yoweri Museveni wa Uganda ujumbe wa maandishi kutoka kwa mwenzake wa Iran.