-
Shamkhani: JCPOA ni mtihani wa kihistoria kwa ufanisi wa taasisi za kimataifa
May 05, 2018 22:06Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema kudumu au kuvunjika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, yakiwa ni makubaliano ya kisiasa na kiusalama yaliyothibitishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ni mtihani wa kihistoria wa kutathmini taathira ya mantiki ya mazungumzo badala ya mizozo na vilevile kiwango cha ufanisi wa taasisi za kimataifa.
-
Indhari ya Russia kuhusu kufutwa makubaliano ya JCPOA na taathira zake mbaya
May 05, 2018 07:39Serikali ya Russia imetoa taarifa ikisisitiza kuwa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA ni utaratibu ulio na mlingano weenye manufaa ya pande zote na kutahadharisha kuwa kuvunjwa makubaliano hayo kutakuwa kwa madhara. Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Russia, kuvurugwa mlingano unaolegalega wa kimaslahi ndani ya makubaliano ya JCPOA kutakuwa na taathira kuu kwa usalama wa kimataifa na muundo unaopiga marufuku uenezaji wa silaha za nyuklia.
-
Ufaransa: Kuihifadhi JCPOA ni kipaumbele chetu, kujitoa ni kutangaza vita
May 05, 2018 03:23Mwakilishi wa kudumu wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, kuyalinda mapatano ya nyuklia ya Iran maarufu kwa jina la JCPOA ndicho kipaumbele cha nchi yake.
-
Russia: Iwapo Marekani itajitoa katika JCPOA, itabidi iwekewe vikwazo
May 05, 2018 03:22Afisa mmoja wa Russia amesisitiza kuwa, kama Marekani itajitoa katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA, itabidi iwekewe vikwazo vya kimataifa.
-
Ujumbe Muhimu wa Zarif kuhusu mapatano ya nyuklia ya Iran + VIDEO
May 04, 2018 12:03Katika Ujumbe wake wa video hapo jana Alkhamisi, Muhammad Jawad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alisema kuwa kuna chaguo moja tu la kufanikisha makubaliano ya nyuklia kati ya Iran na nchi sita kubwa za dunia, nalo ni Marekani kutekeleza ahadi zake zote kuhusiana na makubaliano hayo.
-
Ujumbe wa Zarif: Mapatano ya JCPOA ima yatabakia katika mfumo wake wa sasa au yavunjike kabisa
May 04, 2018 08:08Katika Ujumbe wake wa video hapo jana Alkhamisi, Muhammad Jawad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alisema kuwa kuna chaguo moja tu la kufanikisha makubaliano ya nyuklia kati ya Iran na nchi sita kubwa za dunia, nalo ni Marekani kutekeleza ahadi zake zote kuhusiana na makubaliano hayo.
-
Katibu Mkuu wa UN: JCPOA ni ushindi muhimu wa kidiplomasia
May 04, 2018 02:55Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameonya dhidi ya kuvunjwa makubaliano ya nyuklia ya Iran huku akisisitiza kuwa mapatano hayo ni ushindi muhimu wa kidiplomasia ambayo yanapaswa kulindwa.
-
Malengo mawili ya makelele mapya ya Netanyahu dhidi ya Iran
May 04, 2018 02:20Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni, Jumatatu usiku aliendeleza vitendo vyake vya chuki na ghilba za kisiasa dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuonesha mbele ya kamera za vyombo vya habari vitu alivyodai kuwa eti ni ushahidi kwamba Iran inafanya juhudi za siri za kumiliki silaha za nyuklia.
-
Zarif: Iran haitofanya mazungumzo yoyote kuhusu JCPOA na mapatano hayo hayataongezwa chochote
May 03, 2018 23:42Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika ujumbe alioutoa jana kwa njia ya video kwamba Tehran haitofanya mazungumzo yoyote mapya kuhusu JCPOA na wala mapatano hayo ya nyuklia hayataongezwa chochote. Amesema mapatano hayo yana njia moja tu nayo ni Marekani kuheshimu vipengee vyake vyote.
-
Najafi: Matumizi ya nishati ya nyuklia kwa malengo ya kiraia ni haki ya nchi zote
May 03, 2018 02:20Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia (IAEA) amesisitiza kuwa nchi ambazo zinamiliki mabomu ya nyuklia hazina haki ya kuzuia nchi nyingine zistafidi na teknolojia ya nyuklia kwa malengo ya amani kwa kisingizio cha kuzuia kuenezwa silaha hizo.