-
WFP kupunguza chakula wanachopata wakimbizi nchini Kenya
Oct 03, 2017 00:32Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa WPF, litapunguza kwa asilimia 30 mgao wa chakula kwa wakimbizi 420,000 walio kwenye kambi za Daadab na Kakuma nchini Kenya.
-
Kenya kukabiliana na maandamano ya wapinzani
Sep 29, 2017 11:08Serikali ya Kenya imesema maandamano ya muungano wa upinzani Nasa ambayo yamepangwa kuanza Jumatatu yatadhibitiwa na vitengo vya kuimarisha usalama vya nchi hiyo.
-
Polisi Kenya watawanya wapinzani wanaotaka mabadiliko tume ya uchaguzi
Sep 26, 2017 12:36Polisi wa kuzima ghasia nchini Kenya wametumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wakitaka baadhi ya maafisa wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC wafutwe kazi kabla ya uchaguzi wa rais wa marudio wa Oktoba 26.
-
UN yajitosa katika uchaguzi wa marudio Kenya, wapinzani kuandamana dhidi ya IEBC
Sep 26, 2017 04:20Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) limesaini mkataba na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC) kuhusu zabuni ya karatasi za kupigia kura kwa ajili ya uchaguzi wa marudio wa Oktoba 26.
-
DPP wa Kenya aagiza uchunguzi dhidi ya maafisa wa ngazi za juu wa IEBC
Sep 24, 2017 11:03Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka ya Umma nchini Kenya (DPP), Keriako Tobiko ameagiza polisi na Kamisheni ya Maadili ya Kupambana na Ufisadi EACC kuanzisha uchunguzi dhidi ya maafisa wa ngazi za juu wa Tume ya Uchaguzi nchini humo, kutokana na kasoro zilizojitokeza katika uchaguzi wa mwezi uliopita.
-
Kenya yataka dunia isaidie kikosi cha AMISOM kulinda amani Somalia
Sep 23, 2017 04:43Kenya imeitaka jamii ya kimataifa iongeze zaidi usaidizi wake kwa Kikosi cha Umoja wa Afrika cha Kulinda amani Somalia, AMISOM ili kiweze kushughulikia kwa kina vitisho vya usalama kabla ya kuanza kutekelezwa mpango wa kupunguza idadi ya askari wake.
-
Mwanasheria Mkuu: Kenya haiko kwenye hatari ya mgogoro wa kikatiba
Sep 22, 2017 13:08Mwanasheria Mkuu wa Kenya amesema kuwa nchi hiyo haitakabiliwa na mgogoro wa kikatiba au wa kisiasa hata kama uchaguzi rais wa marudio uliopangwa kufanyika Oktoba 26, umesogezwa tarehe hadi baada ya mwishoni mwa Oktoba.
-
Kenya yachelewesha kuanza vikao vya EALA tangu Juni 2017
Sep 22, 2017 04:34Hatua ya Kenya kutoteua wabunge wake wa Bunge la Afrika Mashariki EALA hadi sasa imechelewesha kuanza vikao vya chombo hicho cha kieneo.
-
Tarehe ya uchaguzi wa marudio Kenya yasogezwa mbele
Sep 22, 2017 04:22Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC) imebadilisha tarehe ya kufanyika uchaguzi wa marudio wa urais hadi Oktoba 26 mwaka huu na wala sio Oktoba 17 kama ilivyotangaza hapo awali.
-
Rais wa Kenya: Hukumu ya Mahakama ya Juu ilikuwa ni "mapinduzi"
Sep 21, 2017 11:15Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema Mahakama ya Juu ya nchi hiyo ilifanya "mapinduzi" dhidi ya matakwa ya wananchi ilipobatilisha matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika mwezi uliopita ambao yeye alishinda.