-
Spika wa Iran akutana na Rais wa Lebanon na Sayyid Nasrullah
Feb 18, 2020 04:22Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Michel Aoun wa Lebanon, Spika wa Bunge la nchi hiyo ya Kiarabu, Nabih Berri na Katibu Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah, Sayyid Hassan Nasrullah mjini Beirut.
-
Kuundwa serikali mpya ya Lebanon; mafanikio na changamoto
Feb 13, 2020 04:39Bunge la Lebanon siku ya Jumanne liliidhinisha baraza jipya la mawaziri la nchi hiyo ambalo lilipendekezwa na Waziri Mkuu Hassan Diab. Baraza hilo lilipitishwa kwa kura 63 za 'ndio' na 20 za 'la' huku mbunge mmoja akijizuia kupiga kura katika kikao hicho kilichohudhuriwa na wabunge 84 kati ya wabunge wote 128 wa Bunge la Lebanon.
-
Hizbullah ya Lebanon: Tutaiunga mkono serikali mpya
Feb 08, 2020 04:29Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbulla ya Lebanon amesema kuwa harakati hiyo itaonyesha imani yake kwa serikali mpya ya nchi hiyo kwa kuwa ina shakhsia wanaofaa.
-
Hizbullah: Marekani ndiyo sababu ya matatizo yote ya Lebanon
Jan 26, 2020 09:26Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema Marekani ndiyo chimbuko la matatizo yote yanayoikabili Lebanon.
-
"ISIS walitaka kushambulia ubalozi wa Marekani Lebanon na kuisingizia Hizbullah"
Jan 24, 2020 02:45Gazeti la al Jamhuriyyah la Lebanon limefichua kuwa, genge la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) lilikuwa limepanga njama za kushambulia ubalozi wa Marekani mjini Beirut ili kuibebesha lawama harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo Hizbullah hasa baada ya Marekani kumuua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds, cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH.
-
Jasusi mmoja wa Marekani atiwa mbaroni mjini Beirut, Lebanon
Jan 20, 2020 09:44Maafisa usalama wa Lebanon wamemtia mbaroni mwandishi mmoja wa habari wa Kimarekani katika maandamano ya wananchi mjini Beirut kwa tuhuma za kuufanyia ujasusi utawala haramu wa Kizayuni.
-
Waziri Mkuu mpya wa Lebanon; vipaumbele vyake na changamoto zinazomkabili
Dec 20, 2019 08:42Rais Michel Aoun wa Lebanon amemtangaza Hassan Diab, shakhsia miongoni mwa Waislamu wa madhehebu ya Sunni na waziri wa zamani wa elimu ya juu wa nchi hiyo, kuwa waziri mkuu mpya na kumpa jukumu la kuunda serikali.
-
Baada ya vuta nikuvute hatimaye Lebanon yapata Waziri Mkuu
Dec 20, 2019 04:33Baada ya vuta nikuvute ya kisiasa nchini Lebanon, hatimaye nchi hiyo imefanikiwa kupata Waziri Mkuu mpya ikiwa ni karibu miezi miwili tangu alipojiuzulu Saad Hariri aliyekuwa akishikilia wadhifa huo.
-
Sheikh Abdul-Amir Qabalan: Mkutano wa Bahrain ni khiana kwa Palestina
Dec 12, 2019 08:38Mkuu wa Baraza Kuu la Kiislamu la Mashia wa Lebanon ameulaani mkutano wa Bahrain na juhudi za kutaka kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel na kusema hatua yoyote ya kutaka kuanzisha uhusiano na Israel ni khiana kwa historia ya Uislamu na ardhi za Palestina.
-
Kuakhirishwa kikao cha Bunge la Lebanon; Saad Hariri katika ndoto za kurejea madarakani
Dec 10, 2019 10:52Jumatatu ya jana tarehe 9 Disemba, ilipangwa kuwa Bunge la Lebanon likutane na kufanya mashauriano kuhusiana na Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo. Hata hivyo kikao hicho cha Bunge kiliakhirishwa.