-
UN yataka mamluki wa kigeni waondoke Libya
Mar 25, 2021 09:30Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya amewataka wapiganaji wote mamluki wa nchi za kigeni kuondoka katika ardhi ya nchi hiyo.
-
Kamanda wa Libya anayesakwa na ICC auawa kwa kupigwa risasi
Mar 25, 2021 03:05Kamanda wa ngazi ya juu huko Libya anayesakwa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC kwa tuhuma za kuhusika na jinai za kivita ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana katika mji wa Benghazi, mashariki mwa Libya.
-
Foreign Policy yafichua taasisi bandia inayodai kuwa na uhusiano na UN, inahusishwa na uhalifu wa kimataifa
Mar 25, 2021 02:34Uchunguzi uliofanywa na gazeti la Foreign Policy umefichua habari za taasisi moja inayodai kuwa na uhusiano na Umoja wa Mataifa na kutetea haki za binadamu ambayo viongozi wake wanatuhumiwa kuhusika na uhalifu na jinai nyingi zikiwemo za kutakatisha fedha chafu na kutorosha mabilioni ya dola za Marekani zilizokuwa zimeporwa kutoroshwa nje ya nchi na kiongozi wa zamani wa Libya, Muammar Gaddafi kabla ya kuuawa kwake.
-
UN: Vikwazo vya silaha dhidi ya Libya havina athari yoyote
Mar 17, 2021 07:31Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wamesema vikwazo vya silaha vya umoja huo dhidi ya Libya vinaendelea kukiukwa na kwa msingi huo havina taathira yoyote.
-
Kuapishwa Serikali ya Muda ya Libya, na changamoto zilizoko mbele yake
Mar 16, 2021 12:57Hatimaye baada ya miezi kadhaa ya mivutano na kuainisha hatima ya siasa za Libya, Mawaziri wa Serikali ya Muda ya Umoja wa Kitaifa waliapishwa jana Jumatatu katika Bunge la nchi hiyo huko katika mji wa Tobruk.
-
Serikali ya muda ya Umoja wa Kitaifa Libya yaapishwa
Mar 16, 2021 02:57Serikali ya muda ya Umoja wa kitaifa ya Libya iliapishwa jana Jumatatu na kuanza rasmi shughuli zake.
-
Serikali mpya ya Libya yaendelea na juhudi za kuikwamua nchi hiyo na migogoro
Mar 14, 2021 02:37Mkuu mpya wa Baraza la Uongozi la Libya amesema kuwa, baraza hilo linafanya juhudi zake zote kwa ajili ya kuikwamua nchi hiyo na migogoro na kuiletea amani ya kudumu, demokrasia, kuheshimishwa haki za binadamu na uhuru wa wananchi wake.
-
UN yataka makubaliano ya usitishaji vita Libya yatekelezwe kikamilifu
Mar 13, 2021 07:35Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetaka pande zinazopigana nchini Libya kutekeleza kikamilifu makubaliano ya usitishaji vita.
-
Italia: Tunaunga mkono juhudi za kuleta amani na utulivu nchini Libya
Mar 12, 2021 12:02Serikali ya Italia imesema kuwa inaunga mkono kikamilifu juhudi za kurejesha amani na utulivu katika nchi ya kaskazini mwa Afrika ya Libya.
-
Wabunge Libya wakutana kujadili baraza la mawaziri
Mar 08, 2021 11:26Wabunge wa pande hasimu nchini Libya wanakutana katika mji wa kistratijia wa Sirte kwa ajili ya kujadiliana kuhusu serikali ya Umoja iliyopendekezwa na Waziri Mkuu Abdul Hamid Dbeibah.