-
Baraza la Usalama la UN launga mkono taarifa ya pamoja ya pande hasimu nchini Libya
Jul 28, 2017 07:32Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeunga mkono kusainiwa hati ya pamoja kati ya pande kuu hasimu nchini Libya kwa lengo la kuinasua nchi hiyo kwenye kinamasi cha mchafukoge.
-
Pirikapirika za Ufaransa za kuwa na nafasi katika nchi iliyogawanyika ya Libya
Jul 27, 2017 11:55Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amekutana na kufanya mazungumzo mjini Paris na viongozi wa pande zinazovutania uongozi wa Libya uliogawanyika.
-
Qatar yakadhibisha madai mapya ya Saudi Arabia
Jul 27, 2017 03:23Mkurugenzi wa Ofisi ya Mawasiliano ya serikali ya Qatar ameyataja madai mapya ya nchi nne za Kiarabu zilizoiwekea Doha vikwazo kuwa ni ya uwongo na yenye kukatisha tamaa.
-
Libya yaialika Italia katika maji yake kupambana na magendo ya binadamu
Jul 26, 2017 14:06Serikali ya Libya yenye makao yake huko Tripoli mji mkuu wa nchi hiyo imezialika meli za kivita za Italia katika maji ya nchi hiyo ili kusaidia mapambano dhidi ya magendo ya binadamu. Hayo yamesemwa leo na Paolo Gentiloni Waziri Mkuu wa Italia.
-
Viongozi hasimu wa Libya wakutana Paris, wakubali kusitisha vita
Jul 26, 2017 03:09Kamanda wa majeshi ya Libya mashariki mwa nchi hiyo, Jenerali Khalifa Haftar na Fayez al Sarraj, Waziri Mkuu wa serikali ya umoja wa kitaifa ya nchi hiyo, magharibi mwa nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika wamekubaliana kusitisha vita kwa masharti.
-
Maiti 13 za wahajiri zapatikana katika boti ya plastiki Libya
Jul 25, 2017 16:30Miili 13 ya wahajiri waliokuwa wakielekea barani Ulaya imepatikana ndani ya boti ya plastiki na wapiga mbizi wa shirika moja lisilo la serikali katika pwani ya Libya.
-
Askari wa gadi ya pwani Libya wawaokoa wahajiri 300
Jul 25, 2017 08:22Kikosi cha gadi ya pwani mwa Libya kimetangaza habari ya kuokolewa wahajiri haramu 300 kutoka katika maji ya pwani mwa nchi hiyo.
-
Askari wa Khalifa Haftar wamewaua wafungwa 20
Jul 25, 2017 02:26Askari wa Khalifa Haftar, kamanda wa Jeshi la Taifa la Libya wamewaua wafungwa 20 kwa tuhuma za kuhusika na kuteka nyara na kutesa askari wa kamanda huyo.
-
Mamia ya maiti za wanachama wa Daesh (ISIS) zimerundikana Libya
Jul 24, 2017 03:47Serikali ya Libya imesema mamia ya maiti za wanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh (ISIS) raia wa kigeni zimerundikana nchini humo, miezi kadhaa baada ya wapiganaji hao kushindwa na vikosi vya serikali katika mji wa Pwani wa nchi hiyo wa Sirte.
-
Libya kuongeza uzalishaji wake wa mafuta
Jul 19, 2017 14:23Viongozi wa Libya wametangaza kuwa nchi hiyo ina mpango wa kuongeza uzalishaji wake wa mafuta hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu na kufikia mapipa milioni moja na laki mbili na eldfu hamsini kwa siku.