-
Waingereza waandamana London kulaani jinai za utawala wa Aal-Saud nchini Yemen
Mar 27, 2017 08:17Mamia ya wakazi wa jiji la London nchini Uingereza, wamefanya maandamano kupinga mashambulizi ya kivamizi ya Saudia nchini Yemen.
-
Wamarekani waandamana Washington dhidi ya lobi ya Kizayuni
Mar 27, 2017 03:16Wanaharakati wanaounga mkono Palestina wamefanya maandamano nje ya ukumbi kunakofanyika kongamano la lobi ya Kizayuni ya Kamati ya Marekani na Israel ya Masuala ya Umma (AIPAC) mjini Washington.
-
Wimbi la maandamano ya wananchi latanda nchini Bahrain dhidi ya utawala wa Aal-Khalifah
Mar 25, 2017 22:10Maeneo tofauti ya Bahrain yamekumbwa na wimbi la maandamano makubwa ya wananchi wanaopinga hukumu za adhabu ya kifo zilizotolewa na mahakama za kimaonyesho za nchi hiyo na kadhalika kutangaza uungaji mkono wao kwa Mustafa Hamdan, kijana aliyeuawa shahidi na askari wa utawala wa Aal-Khalifah.
-
Wapinzani waandamana Zimbabwe, wadai kuna njama za kuiba kura
Mar 22, 2017 11:12Maelfu ya wafuasi wa vyama vya upinzani nchini Zimbabwe wameshiriki maandamano katika mji mkuu Harare, kulalamikia kile wanachodai kuwa ni njama ya kuiba kura katika uchaguzi ujao wa rais.
-
Wanawake Yemen waandamana nje ya ofisi za UN kulaani jinai za Saudia
Mar 15, 2017 03:29Wanawake wa Yemen wamefanya maandamano na kukita kambi nje ya ofisi za Umoja wa Mataifa katika mji mkuu Sana’a, kuutaka umoja huo usitishe jinai na uvamizi wa Saudi Arabia dhidi ya nchi hiyo.
-
Wapalestina waandamana kupinga marufuku ya adhana Quds tukufu
Mar 12, 2017 03:52Maelfu ya wananchi wa Palestina inayokaliwa kwa mabavu wamefanya maandamano kulaani sheria iliyopasishwa hivi karibuni na Bunge la Israel ya kupiga marufuku adhana katika mji mtakatifu wa Quds.
-
Wamisri waandamana nchi nzima dhidi ya serikali kulalamikia kuwekwa mgao wa mikate
Mar 09, 2017 04:22Raia wa Misri wamefanya maandamano dhidi ya serikali katika mikoa tofauti ya nchi hiyo, kulalamikia hatua ya kuwekwa mgao katika upatikanaji wa mikate nchini humo.
-
Wafuasi na wapinzani wa Trump watwangana makonde nchini Marekani
Mar 05, 2017 04:09Habari kutoka nchini Marekani zinasema kuwa kumezuka mapigano baina ya wafuasi na wapinzani wa Donald Trump katika mji wa Berkeley wa jimbo la California, magharibi mwa nchi hiyo.
-
Wananchi wa Yemen waandamana tena dhidi ya Saudia
Mar 04, 2017 04:03Makumi ya maelfu ya wananchi wa Yemen kwa mara nyingine tena wamejitokeza mabarabarani kushiriki maandamano ya kulaani uvamizi na hujuma za kijeshi za utawala wa Saudi Arabia.
-
Maandamano makubwa ya kuwaunga mkono wahajiri yafanyika Uhispania
Feb 19, 2017 04:10Katika hali ambayo Rais Donald Trump wa Marekani anatazamiwa wiki ijayo kutangaza 'sheria kali zaidi' za kudhibiti wahajiri na raia wa nchi saba za Kiislamu, mamia ya maelfu ya wananchi wamefanya maandamano Uhispania kuonyesha uungaji mkono wao kwa wajahiri.