Wamarekani waandamana Washington dhidi ya lobi ya Kizayuni
https://parstoday.ir/sw/news/world-i26914-wamarekani_waandamana_washington_dhidi_ya_lobi_ya_kizayuni
Wanaharakati wanaounga mkono Palestina wamefanya maandamano nje ya ukumbi kunakofanyika kongamano la lobi ya Kizayuni ya Kamati ya Marekani na Israel ya Masuala ya Umma (AIPAC) mjini Washington.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 27, 2017 03:16 UTC
  • Wamarekani waandamana Washington dhidi ya lobi ya Kizayuni

Wanaharakati wanaounga mkono Palestina wamefanya maandamano nje ya ukumbi kunakofanyika kongamano la lobi ya Kizayuni ya Kamati ya Marekani na Israel ya Masuala ya Umma (AIPAC) mjini Washington.

Habari zinasema kuwa, aghalabu ya walioshiriki maandamano hayo ni wanaharakati wa mrengo wa kushoto wa vuguvugu la Jewish Resistance.

Waandamanaji hao wamekosoa vikali sera za Rais Donald Trump wa Marekani za kuuunga mkono utawala wa Kizayuni wa Israel sambamba na kulaani upanuzi wa vitongoji vya walowezi za Kiyaudi katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.

AIPAC

Yonah Lieberman, mmoja wa wanaharakati waliondaa maandamano hayo wa asasi inayopinga kuendelezwa ujenzi wa vitongi vya walowezi iitwayo IfNotNow amesema kuwa: "Tunaandamana kupinga AIPAC, licha ya kuwa Myahudi anayeishi Marekani, hakumaanisha kuwa tunaunga mkono vitendo vya kikatili wanavyofanyiwa Wapalestina na Tek Aviv."

Lobi hiyo yenye ushawishi mkubwa ya AIPAC imekuwa ikisisitiza kuwa, katu haitalegeza misimamo yake ya kuishinikiza serikali ya Washington kuiwekea vikwazo zaidi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.