-
Bahrain yasisitiza kuwanyonga wanaharakati 3 wa Kishia
Jun 01, 2016 02:32Mahakama ya Rufaa ya Bahrain imekataa kutengua hukumu ya kunyongwa wanaharakati watatu wa Kiislamu wa madhehebu ya Shia.
-
5 wahukumiwa maisha jela Uganda kwa mashambulizi ya kigaidi Kampala
May 28, 2016 03:21Mahakama Kuu ya Uganda imewahukumu kifungo cha miaka mitano jela, watu watano miongoni mwa wanane waliopatikana na hatia ya kuhusika katika mashambulizi pacha mjini Kampala, wakati wa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2010.
-
Rais wa Afrika Kusini akata rufaa juu ya kesi za ufisadi dhidi yake
May 24, 2016 11:50Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ametangaza kuwa atakata rufaa kupinga kufufuliwa kesi za ufisadi wa kifedha dhidi yake.
-
Misri yatoa hukumu dhidi ya 152 waliopinga Saudia kupewa visiwa vya nchi hiyo
May 15, 2016 09:11Mahakama moja nchini Misri imewahukumu watu 152 kifungo cha kati ya miaka miwili hadi mitano jela kwa kushiriki maandamano ya Aprili 25 ya kupinga hatua ya serikali ya nchi hiyo kuipa Saudi Arabia visiwa viwili, vinavyomilikiwa na nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.
-
Mahakama ya kilele DRC: Kabila kusalia uongozini hata baada ya muhula wake kumalizika
May 12, 2016 02:19Mahakama ya Juu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imesema kuwa huenda Rais Joseph Kabila wa nchi hiyo akasalia madarakani hata baada ya kumalizika muhula wake iwapo uchaguzi mkuu utakosa kufanyika mwezi Novemba mwaka huu.
-
21 wahukumiwa kifungo cha maisha jela Burundi kwa 'kupanga mapinduzi'
May 10, 2016 02:25Mahakama ya Juu ya Burundi imetoa hukumu ya maisha jela kwa maafisa 21 wa jeshi la nchi hiyo, wanaodaiwa kuhusika na njama iliyofeli ya kuipindua serikali mwezi Mei mwaka jana wa 2015.
-
Arab League: Kuundwe mahakama maalumu ya jinai za Israel
Apr 21, 2016 10:52Jumuiya ya Nchi za Kiarabu imetoa mwito wa kuundwa mahakama maalumu ya jinai kwa ajili ya kuwapandisha kizimbani Wazayuni kutokana na hatua yao ya kukiuka haki za Wapalestina.
-
Rais wa Misri kotini kwa kuipa Saudia visiwa vya Sanafir na Tiran
Apr 20, 2016 03:13Chama kimoja cha upinzani nchini Misri kimempelekea mahakamani Rais Abdul Fattah al-Sisi wa nchi hiyo kufuatia uamuzi wake wa kukabidhi umiliki wa visiwa viwili vya kiistratejia kwa utawala wa Saudi Arabia.
-
Mahakama: Rais Zuma alikiuka katiba, arejeshe fedha zilizofujwa
Mar 31, 2016 09:42Mahakama ya Juu ya Afrika Kusini imemuagiza Rais Jacob Zuma wa nchi hiyo kuirejeshea serikali sehemu ya dola milioni 16 za Marekani zilizotumika kukarabati makazi yake binafsi, kwenye moja ya kashfa kubwa za ufisadi zilizowahi kuripotiwa nchini humo katika miaka ya hivi karibuni.
-
Mahakama ya Juu Uganda yatupilia mbali kesi ya kupinga ushindi wa Museveni
Mar 31, 2016 09:33Mahakama ya Juu ya Uganda imetupilia mbali kesi iliyowasilishwa na Waziri Mkuu wa zamani nchini humo Amama Mbabazi ya kupinga ushindi wa Rais Yoweri Museveni katika uchaguzi wa rais wa Februari mwaka huu.