-
Rais wa Tunisia avunja Baraza Kuu la Idara ya Mahakama
Feb 07, 2022 02:31Rais Kais Saied wa Tunisia ametangaza habari ya kulivunja Baraza Kuu la Idara ya Mahakama, huku msuguano mkali ukiendelea kushuhudiwa baina yake na mhimili huo wa dola.
-
Rais wa Gambia awataka wapinzani waheshimu uamuzi wa mahakama
Dec 29, 2021 07:44Rais Adama Barrow wa Gambia ametoa mwito kwa upinzani nchini humo kukubali na kuheshimu uamuzi wa jana Jumanne wa Mahakama ya Juu ya nchi hiyo wa kutupilia mbali kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais yaliyompa ushindi kiongozi huyo.
-
Kuendelea ubaguzi wa rangi Marekani
Nov 23, 2021 08:11Uamuzi wa mahakama ya Marekani wa kufutilia mbali mashtaka ya mauaji yaliyokuwa yanamkabili kijana mmoja mweupe aliyehusika na mauaji ya watu wawili katika maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi nchini humo mwaka uliopita, kwa mara nyingine umeamsha hasira ya wengi katika nchi hiyo ya Magharibi.
-
Mwanahabari wa Marekani ashitakiwa kwa ugaidi Myanmar
Nov 10, 2021 14:23Mwandishi wa habari wa Marekani ambaye anazuiliwa na vyombo vya usalama nchini Myanmar kwa miezi kadhaa sasa amefunguliwa mashitaka ya ugaidi na uhaini, na yumkini akahukumiwa kifungo cha maisha jela.
-
Majasusi wa Israel wahukumiwa kifo Ukanda wa Gaza
Oct 29, 2021 03:47Vyombo vya habari vya Palestina vimeripoti kuwa, Mahakama ya Kijeshi ya Ukanda wa Gaza imewahukumu kifo majajusi sita wa utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Serikali ya Canada yahukumiwa kuwalipa fidia wakazi asili wa nchi hiyo
Oct 01, 2021 05:11Mahakama ya Haki za Binadamu ya Canada ambayo mwaka 2016 iliituhumu serikali ya nchi kuwa imefanya ubaguzi wa kimbari, kutumia mabavu na kuua Wahindi Wekundu wenyeji wa nchi hiyo imeitaka serikali ya Ottawa kuwalipa fidia Wahindi Wekundu kwa kupatikana na hatia ya kukiuka haki zao za kibinadamu
-
Palestina yataka kuharakishwa kesi ya kuchunguza uhalifu wa Israel mahakama ya ICC
Sep 05, 2021 07:19Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Palestina imetoa wito wa kuharakishwa mwenendo wa kesi ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) huko Hague nchini Uholanzi kwa ajili ya kuchunguza jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina.
-
Wafuasi wa chama cha upinzani Tanzania Chadema wakamatwa wakiimba "Mbowe sio gaidi"
Aug 05, 2021 12:33Wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambacho ni chama kikuu cha upinzani Tanzania waliokuwa wamekusanyika nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kuzuiwa kuingia ndani ya korti wamekamatwa na wanashikiliwa na Jeshi la Polisi.
-
Wanasheria Tanzania wataka Mbowe ama aachiwe au afikishwe mbele vyombo vya sheria
Jul 25, 2021 11:29Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), kimeingilia kati sakata la kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, kikitaka kiongozi huyo wa upinzani Tanzania ama aachiliwe huru au afikishwe kwenye mamlaka za kisheria.
-
Mahakama Afrika Kusini yamhukumu Zuma zaidi ya mwaka mmoja jela
Jun 30, 2021 02:25Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, ambaye kesi yake ya ufisadi inaendelea, amehukumiwa kifungo cha miezi 15 gerezani kwa kudharau korti.