-
Muhusika mkuu wa mauaji ya ndugu ya Katibu Mkuu wa Answarullah aangamizwa
Sep 11, 2019 23:46Wizara ya Mambo ya Ndani ya Serikali ya Wokovo wa Kitaifa nchini Yemen imesema kuwa, Mohammad Ali Ghayd Zawi, muhusika mkuu wa mauaji ya Ibrahim Badruddin Al Houthi, ndugu ya Katibu Mkuu wa Harakati ya Wananchi ya Answarullah nchini Yemen ameangamizwa.
-
Afrika Kusini yakiri: "Afrophobia" inahusika katika hujuma zinazowalenga raia wa kigeni
Sep 05, 2019 08:16Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini amesema kuwa tabia ya kujichukulia sheria mkononi dhdi ya raia wa nchi nyingine za Afrika wanaoishi nchini humo ni moja kati ya sababu za mashambulizi na hujuma zinazowalenga wafanyabiashara wa nchi za kigeni katika miji mbalimbali ya nchi hiyo.
-
Vinara wa jaribio la mapinduzi Burkina Faso wahukumiwa kifungo cha miaka 20 jela
Sep 02, 2019 22:37Waitifaki wawili wakubwa wa rais aliyeondolewa madarakani nchini Burkina Faso, Blaise Compaore, wamehukumiwa vifungo vya hadi miaka 20 jela kwa kupatikana na hatia ya kupanga mapinduzi ya mwaka 2015 dhidi ya serikali ya mpito nchini humo.
-
Yemen yawakamata mamluki waliomuua Ibrahim al Houthi
Aug 10, 2019 03:10Idara za intelijensia nchini Yemen zimefanikiwa kuwakamata mamluki waliomuua Ibrahim Badreddin al Houthi, kaka yake Katibu Mkuu wa Harakati ya Ansarullah.
-
FBI yatahadharisha, wapinzani wa utawala wa Saudia wako hatarini kuuawa
Jul 13, 2019 21:48Polisi ya Federali nchini Marekani FBI imetahadharisha kwamba, wapinzani wa utawala wa kifalme wa Saudi Arabia na jamaa wa Jamal Khashoggi wanakabiliwa na hatari ya kuuawa.
-
Wanajeshi 18 wa Niger wauawa katika hujuma dhidi ya kambi yao
Jul 02, 2019 07:30Kwa akali askari 18 wameuawa baada ya watu waliojizatiti kwa silaha kushambulia kambi ya jeshi magharibi mwa Niger.
-
Maduro: Jaribio lililofeli la kutaka kuniua liligharimu dola milioni 20
Jun 19, 2019 22:14Rais wa Venezuela amemtuhumu mbunge mmoja wa upinzani kwa kuiba kitita kikubwa cha fedha ili kutekeleza njama ya mauaji dhidi yake mwezi Agosti mwaka jana.
-
Waandamanaji waliouawa na maafisa usalama Sudan wapindukia 108
Jun 06, 2019 02:07Idadi ya watu waliouawa katika wimbi jipya la ukatili na utumiaji wa nguvu kupita kisiasa wa maafisa usalama wa Sudan dhidi ya waandamanaji wanaotaka kukabidhiwa madaraka kwa utawala wa kiraia imepindukia watu 100.
-
Mchumba wa Khashoggi akosoa kimya cha Marekani kwa mauaji ya mwanahabari huyo wa Saudia
May 17, 2019 02:56Mchumba wa Jamal Khashoggi, mwandishi habari mkosoaji wa utawala wa Aal-Saud aliyeuawa ndani ya ubalozi mdogo wa Saudi Arabia mjini Istanbul, Uturuki mwaka jana ameitaka Marekani kuanzisha uchunguzi wa mauaji ya kutisha ya mpenzi wake huyo ambaye alikuwa amepanga kufunga naye ndoa kabla ya kuuawa.
-
UN: Watu 56 wameuawa katika mapigano yanayoendelea Libya
Apr 11, 2019 09:28Umoja wa Mataifa umesema mapigano kati ya vikosi vya Serikali ya Maafikiano ya Kitaifa na vile vinavyoongozwa na Jenerali Khalifa Haftar nchini Libya yamesababisha watu 56 kupoteza maisha kufikia sasa.