Watu 8 wauwa karibu na mbuga ya wanyama nchini Rwanda
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i56437-watu_8_wauwa_karibu_na_mbuga_ya_wanyama_nchini_rwanda
Watu wanane wameuawa katika shambulizi la watu waliobeba silaha karibu na mbuga ya wanyama ya Volcanoes kaskazini mwa Rwanda.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 05, 2019 10:59 UTC
  • Watu 8 wauwa karibu na mbuga ya wanyama nchini Rwanda

Watu wanane wameuawa katika shambulizi la watu waliobeba silaha karibu na mbuga ya wanyama ya Volcanoes kaskazini mwa Rwanda.

Msemaji wa polisi, John Bosco Kabera amesema leo Jumamosi kuwa, mauaji hayo yalitokea usiku wa kuamkia leo katika eneo la Kinigi wilayani Musanze, eneo ambalo ni mashuhuri kama kitovu cha utalii nchini humo.

Amesema, "majambazi hao wameua watu wanane, ambapo wawili wameuawa kwa kupigwa risasi na sita wameuawa kwa silaha butu. Watu 18 wamejeruhiwa na wanaendelea kupatiwa matibabu."

Waasi wa FDLR wanaofanya mauaji Rwanda na DRC

Polisi ya Rwanda haijaainisha iwapo watalii ni miongoni mwa watu waliouawa katika shambulizi hilo. Msemaji wa polisi, John Bosco Kabera ameongeza kuwa, maafisa usalama wanafanya msako mkali wa kuwatafuta na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria wahalifu hao.

Haijabainika iwapo waliotenda jinai hiyo ni raia wa Rwanda au wapiganaji wenye mfungamano na kundi la waasi la FDLR la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambalo lina historia ya kutekeleza uhalifu wa kuvizia nchini Rwanda.