20 wauawa katika shambulizi dhidi ya mgodi wa dhahabu Burkina Faso
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i56449-20_wauawa_katika_shambulizi_dhidi_ya_mgodi_wa_dhahabu_burkina_faso
Kwa akali watu 20 wameuawa baada ya watu waliobeba silaha kushambulia mgodi wa dhahabu kaskazini mwa Burkina Faso.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 06, 2019 04:39 UTC
  • 20 wauawa katika shambulizi dhidi ya mgodi wa dhahabu Burkina Faso

Kwa akali watu 20 wameuawa baada ya watu waliobeba silaha kushambulia mgodi wa dhahabu kaskazini mwa Burkina Faso.

Duru za habari zinaarifu kuwa, watu wasiojulikana ambao walikuwa wamejizatiti kwa silaha wamevamia mgodi huo katika kijiji cha Madudaji katika mkoa wa Sam kaskazini mwa nchi na kutekeleza ukatili huo.

Vyombo vya usalama katika eneo hilo vimeripoti kuwa, watu wengine kadhaa wamejeruhiwa katika hujuma hiyo ya kuvizia.

Wiki iliyopita, watu 20 waliuawa katika mashambulizi mawili tofauti ya watu waliokuwa juu ya pikipiki katika mikoa ya Bam na Sam kaskazini mwa Burkina Faso.

Maafisa usalama katika operesheni Burkina Faso

Serikali ya Burkina Faso kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu hadi sasa imetangaza hali ya hatari katika majimbo saba kati ya 13 ya nchi hiyo. 

Mamia ya watu wameuawa katika mashambulizi ya makundi ya kigaidi na magenge ya waasi wanaobebe silaha nchini Burkina Faso tangu mwaka 2015 hadi sasa.