Jun 28, 2021 10:26
Huku awamu ya pili ya kujazwa maji katika Bwawa la An Nahda (Grand Renaissance Dam-GERD-) la Ethiopia katika Mto Nile ikikaribia, Misri na Sudan, nchi mbili ambazo zinapinga ujenzi wa bwawa hilo, zimetaka ujazwaji maji huo usitishwe kwa muda. Nchi hizo mbili zimetaka Ethiopia izipatie dhamana kuwa haki zao zitalindwa, jambo ambalo limeibua taharuki mpya baina ya nchi hizo tatu.