-
Mkuu wa genge la Boko Haram ajipiga risasi kutaka kujiua Nigeria
May 22, 2021 02:05Serikali na jeshi la Nigeria limethibitisha habari zinasosema kuwa, Abubakar Shekau, mkuu wa genge la kigaidi na ukufurishaji la Boko Haram amejipiga risasi begani katika jaribio la kutaka kujiua. Hii ni katika hali ambayo vyombo vingi vya habari vimeripoti kuwa, Shekau amejiua.
-
Wanachama wa Harakati ya Kiislamu Nigeria washiriki matembezi ya Siku ya Quds
May 08, 2021 07:51Wanachama wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria jana Ijumaa walijitokeza kwa wingi katika matembezi ya Siku ya Kimataifa ya Quds katika miji mikubwa ya nchi hiyo ya Afrika Magharibi.
-
Bunge la Nigeria lataka kushughulikiwa tatizo la ukosefu wa usalama unaoikabili nchi
Apr 29, 2021 03:35Bunge la Nigeria limepasisha maazimio kadhaa yanayomtaka Rais wa nchi, vikosi vya ulinzi na jeshi la polisi nchini humo kushughulikia tatizo la ukosefu wa usalama katika baadhi ya majimbo ya nchi hiyo ambalo limekuwa likiyatesa maeneo hayo kwa miaka kadhaa sasa.
-
Askari usalama Nigeria wawakamata wanachama 40 wa genge lenye silaha
Apr 27, 2021 02:46Kikosi cha usalama nchini Nigeria ckimewatia nguvuni wanachama 40 wa genge la watu waliokuwa na silaha wakati wa operesheni iliyofanyika katika jimbo la kusini la Edo.
-
Polisi ya Nigeria yaua 'majambazi' 30 kaskazini magharibi mwa nchi
Apr 21, 2021 01:50Jeshi la Polisi la Nigeria limetangaza kuwa limeua wabeba silaha 30, baada ya genge la majambazi kuvamia vijiji vinne huko kaskazini magharibi mwa nchi.
-
Nigeria yatuma makumi ya askari polisi wake nchini Somalia
Apr 19, 2021 03:17Kikosi cha askari polisi 144 wa Nigeria kimewasili nchini Somalia, kwenda kupiga jeki jitihada za kurejesha uthabiti katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.
-
Watekaji nyara watishia kuua makumi ya wanafunzi wa Nigeria
Apr 18, 2021 22:23Genge la wabeba silaha lililoteka wanafunzi karibu 30 wa taasisi moja ya elimu ya juu katika jimbo la Kaduna huko kaskazini magharibi mwa Nigeria mwezi uliopita limetishia kuwaua vijana hao wa kike na kiume, baada ya serikali kukataa kuwapa kikomboleo.
-
Wanigeria wataka kuachiwa huru Sheikh Ibrahim Zakzaky
Apr 17, 2021 03:05Mamia ya wafuasi wa Harakati ya Kiislamu Nigeria (IMN), wamefanya maandamano wakitaka kuachiwa huru kiongozi wa harakati hiyo, Sheikh Ibrahim Zakzaky na mkewe, Mallimah Zeenah.
-
Raia 65,000 wahama makazi yao kaskazini mashariki ya Nigeria kukimbia mashambulio ya kundi la ISWAP
Apr 16, 2021 22:12Shirka la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR limeripoti kuwa, watu wasiopungua 65,000 wameuhama mji wa Damasak kaskazini mashariki ya Nigeria kufuatia mashambulio kadhaa ya kundi la wabeba silaha.
-
Watu wenye silaha wauwa wanajeshi 11 katika jimbo la Benue, Nigeria
Apr 09, 2021 11:04Msemaji wa jeshi la Nigeria amesema kuwa wanajeshi wa nchi hiyo waliokuwa wakifanya kazi jimbo la Benue katikati mwa nchi hiyo wameshambuliwa na watu wenye silaha wakiwa kazini.