-
Mgombea wa upinzani Nigeria kuzingatia msamaha kwa washukiwa wa ufisadi iwapo atachaguliwa kuwa Rais
Jan 31, 2019 11:24Atiku Abubakar mgombea wa upinzani wa kiti cha urais katika uchaguzi wa mwezi ujao nchini Nigeria amesema kuwa atazingatia suala la kuwapa msamaha washukiwa wa ufisadi nchini humo lengo likiwa ni kusaidia kurejeshwa nchini mabilioni ya dola yaliyofichwa nje ya nchi na wanasiasa na maafisa wa serikali.
-
Mahakama Nigeria yataka jopo lisikize kesi dhidi ya Jaji Mkuu aliyesimamishwa kazi
Jan 30, 2019 11:12Mahakama ya Rufaa nchini Nigeria hii leo imetoa uamuzi wa kutaka jopo la uchunguzi lisikilize kesi inayomuandama Jaji Mkuu wa nchi hiyo aliyesimamishwa kazi hivi karibuni.
-
UN: Tishio la Boko Haram Nigeria lasababisha watu 30 elfu kutoroka nchi
Jan 29, 2019 12:41Umoja wa Mataifa umesema watu zaidi ya 30,000 wamekimbia makazi yao katika mji wa Rann kaskazini mwa Nigeria na kuingia katika nchi jirani ya Cameroon kutokana na wasiwasi wa kushambuliwa na wanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram.
-
Boko Haram: Tumeua askari 30 kaskazini mashariki mwa Nigeria
Jan 28, 2019 04:40Kundi la kigaidi na ukufurishaji la Boko Haram limedai kuwa wanachama wake wametekeleza shambulizi katika eneo la kaskazini mashariki mwa Nigeria na kuua askari 30 wa nchi hiyo.
-
Nigeria yapinga uingiliaji wa nchi za kigeni katika masuala yake ya ndani
Jan 27, 2019 23:59Serikali ya Nigeria imetangaza kuwa, haitakubali uingiliaji wa nchi za kigeni katika masuala yake ya ndani.
-
Upinzani Nigeria wasimamisha kampeni baada ya kutimuliwa Jaji Mkuu
Jan 26, 2019 04:54Chama kikuu cha upinzani nchini Nigeria kimetangaza kufuta kampeni zake kwa muda wa masaa 72 kulalamikia hatua ya serikali ya Rais Muhammadu Buhari ya kumsimamisha kazi Jaji Mkuu wa nchi hiyo.
-
Wimbi jipya la wakimbizi laibuka kaskazini mashariki mwa Nigeria kufuatia kuongezeka machafuko
Jan 24, 2019 00:36Msemaji wa Umoja wa Mataifa ametangaza kuwa, kufuatia kuongezeka machafuko kaskazini mashariki mwa Nigeria, kwa mara nyingine tena makumi ya maelfu ya raia wamelazimika kuwa wakimbizi katika maeneo hayo.
-
Waislamu Nigeria washinikiza kuachiwa huru mwanahabari Marzieh Hashemi
Jan 22, 2019 04:26Waislamu na wanaharakati wa kutetea haki za binadamu nchini Nigeria wamefanya maandamano kulaani kukamatwa na kuwekwa kizuizini nchini Marekani Marzieh Hashemi, mwandishi wa habari na mtangazaji wa kanali ya kimataifa ya Press TV ya Iran.
-
Mapigano ya watu wenye silaha yashtadi kaskazini mashariki mwa Nigeria
Jan 19, 2019 04:03Makundi yenye silaha yamezidisha mashambulizi yao nchini Nigeria ambapo katika kipindi cha wiki tatu zilizopita zaidi ya askari 100 wa nchi hiyo wameuawa au kutekwa nyara.
-
Makumi wapoteza maisha katika mripuko wa lori la mafuta Nigeria
Jan 13, 2019 00:08Makumi ya watu wanahofiwa kupoteza maisha katika mripuko wa lori la mafuta katika eneo la Odukpani, jimboni Cross River kusini mashariki mwa Nigeria.